PATANISHO: Mke wangu ndiye alifanya nilete wanawake kwa nyumba

Bwana Raphael alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Judith akisema alipata ametoweka bila ya wawili hao kukosana.

Baada ya kuishi na mke wangu vyema, shida kati yetu ilianza mwaka wa 2014 wakati kulikuwa na tetesi kuwa ana mpango wa kando na mchungaji wetu.

Tuliketi chini na kuzungumza kwani tulifikiria kuwa huenda ilikuwa tu maneno ya watu lakini siku moja nilipata amefunganya virago vyake na nikimuuliza huwa hanijibu.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa tangu 1997 na wamejaliwa watoto watatu ila mmoja alifariki.

Wewe mbona huwaambii maneno yako ya kuleta wanawake kwa nyumba? Aliuliza bi Judith. Kama unataka kuleta mwingine leta tu juu umezoea kuleta mabibi za wengine. Aliuliza Judith.

Hata hivyo Raphael alijitetea kuwa mkewe ndiye alimsukuma kuleta wanawake wengine kwa nyumba na kuwa hakuwaleta kwa raha ila wawili hao hawakuwa na furaha baada ya kutengwa kwa miezi mitano.

Unajua mtu akifanya mara ya kwanza ni mistake lakini ilifika wakati anapatia mke wa watu anitusi na hiyo ni uchungu. Aliongeza Judith.