PATANISHO: NDOA YA UNYAMA!!,Mume wangu alinichapa hadi mimba kuharibika-Milly

Katika kitengo cha patanisho mwana dada mmoja anayefahamika kama Milly alituma ujumbe na kusema  wa kutaka kupatanishwa na mumewe Joseph Kimanzi baada ya kupokea kichapo mithili ya mbwa na alichosingiziwa na majirani wake .

" Nilibahatika na kupata mume, alipokua akitoka kazi anaambiwa na jirani kua ameniona na wanaume huko nje, akiniuliza na nika mwambia ni uongo

Alinichapa mara ya kwanza hadi akachukua jiwe akanichapa nikiwa na mimba mpaka mimba ikatoka, baada ya hapo aliniomba msamaha tukarudiana

Sasa juzi alinichapa kwa sababu ya maneno tena ya uongo nilienda jana nikaenda kupimwa nikaambiwa nina mimba, nataka tupatanishwe ili turudiane

Nina umri wa miaka,23, na mume wangu pia ana umri huohuo." Milly Alieleza.

Wawili hao wamekaa kwa ndoa  mwaka mmoja na alipopigiwa simu bwanake Joseph an kusikia sauti ya mukewe alikataa katakata kuzungumza na kuzima simu.

Milly alisema kuwa amekuwa akipokea kichapo hicho kutoka kwa mumewe miaka hiyo yote na kugaidi kuwa atajukumika na kuwalea wanawe kama mama mzazi pasi na usaidizi kutoka kwa janadume  kwa jina Joseph.