PATANISHO: Nataka mpango wa kando akubalike kama mke wa pili

John alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Margaret, akisema walikosana kwa ajili ya mpango wa pili.

"Tumekosana kidogo baada yake kulalamika kuwa nilikuwa na mpango wa kando na yule msichana alikuwa kwao na alipigiwa simu kuwa ex wangu amerudi na hapo akanuna.

Alikujia watoto na kuchukua vitu kadhaa na kwenda nyumbani." Alieleza John akisema aliwachia mtoto mmoja huku mkewe akienda na wawili.

"Ningependa arudi kwani tumekuwa tukiishi vyema licha ya huyu mpango wa kando" Alisimulia akidai wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 11.

Margaret alikiri kuwa mumewe alimpeleka ushago na mwezi huo huo aligundua kuwa ana mke mwingine ambaye alimkodishia nyumba.

"Watu walikuwa wananiambia ana mke mwingine na ana mimba na nikaamua kufunga safari nikajionee. Imagine tumeisha na huyo mwanaume miaka kumi na moja na hajawahi kanyaga kwetu." Alisema Margaret.

Upande wake John alikuwa analalamikia tu mtoto wake bila kujali alichomfanyia mkewe.

"Bwana Gidi shame on me kwa sababu na regret kwani nilijipata tu." Alijitetea John huku Maggy akikiri kuwa hawezi kubali kuletewa mke wa pili kwani hajawahi kalishwa chini na kuelezwa kuhusu lile.

Hata hivyo, alisisitiza bwana John asafiri hadi nyumbani kwao na mzazi wake ili wazungumze kwani hajawahi kanyaga kwa wakwe zake hata mara moja.