PATANISHO: Nilimeza Sumu Baada Ya Mke Wa Kwanza Kutoweka

George alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Benedicte.

"Tulioana na huyu mwanamke na tumeisha kwa mwaka mmoja na nusu na tumeishi tu tukisumbuana.

Enyewe tulipokosana nikaoa mke mwingine lakini tukakosana na hapo nikaamua kumrudisha yule mwingine, na nikamueleza kuwa nilikuwa nimeoa mke mwingine." Alisimulia George.

Sasa walipopatana wawili yule wa kwanza akapotea na kuolewa hapo tu kando yangu.

Sasa niligadhabishwa na yale na nikaamua kunywa sumu. Nikalazwa hospitalini na nilipopona nikapata hata mke wa pili ametoweka akidai hanitaki tena. Sasa nimechanganikiwa lakini namtaka yule mke wa kwanza ambaye tumejaliwa pamoja watoto wawili." Aliongeza George aliye na miaka 23.

Mkewe ana umri wa miaka ishirini.

Kulingana na Benedict, alikasirishwa na hatua ya bwana George kumleta mwanadada mwingine nyumbani mwao.

"Aliniletea mwanamke kwa nyumba na hapo nikaamua kutoka kwani walianza kunionesha madharau. Alikuwa amenidanganya kuwa hakuna mwanadada mwingine na hapo nikampata huyo mwanadada na sikuwa na lakufanya ila kuondoka." Alisema.

Umezoea kuniambia nikusamehe lakini nikirudi unanionesha madharau, mimi hapo sitarudi fanya kazi yako. Mimi nitachunga watoto lakini sitarudi." Alimueleza George.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be