PATANISHO: Nilitumiwa picha ya kifua na mwanadada Facebook

patanisho.Ghost
patanisho.Ghost
Nawachwa! Hicho ndicho kilikuwa kilio chake bwana Philip aliyeomba kupatanishwa na mkewe bi Reggie, akisema mwanadada fulani kupitia mtandao wa Facebook alimtumia picha ya kifua chake.

Philip aliomba ndoa yake ya miaka minne iokolewe.

Kuna msichana ambaye tumekuwa tukizungumza naye Facebook kwa siku mbili na jana nikitoka kazini mke wangu alinitolea simu na kuwekelea mezani. Picha yenyewe ni ya mwanadada ambaye alikuwa uchi na mimi simjui hata kidogo.

Isitoshe amekuwa akinishuku kwani nikienda kwa jamii yangu yeye hudhani naenda kutafuta wanadada.

Philip, 32, na mkewe, 26, wamejaliwa na mtoto mmoja na anasema shida ni kuwa mkewe sio wa kutoka kabila lake.

Tulijaribu kumfikia bi Reggie lakini hatukufua dafu. Ilibidi tumpe Philip nafasi ajitetee kwa mkewe na aliapa kutoka katika mitandao yote ya kijamii ili kujenga ndoa yake.

Kama unaniskiza, hayo makosa yamefanyika mara moja tu na hata hiyo app ya Facebook nitafuta leo na sitarudi huko tena. Usije ukaniwacha kwa ajili ya kosa moja na nakuomba unisamehe, mimi nakupenda sana kama mrenda.

Je una mawaidha gani kwa bwana Philip kuhusu anayopitia?