ghost son

PATANISHO: Siwezi ishi boma la mzee ambapo nadharauliwa

Tom, mwenye umri wa miaka 57, ndiye aliyeomba kupatanishwa mkewe Noel, 45 akisema wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita.

“Tulipatana na mke wangu jiji la Nairobi na nilikuwa na watoto baada ya mke wa kwanza kuondoka na kuolewa mahala kwingine. Sasa mke wangu anaishi ushago na kila mara naenda huko mimi hupata amefunganya virago na kuondoka. Amefanya hivo mara mbili sasa.” Tom alisema.

PATANISHO: Nilitumiwa picha ya kifua na mwanadada Facebook

Aliongeza,

Nilipomuuliza alikiri kuwa hawezani na mambo ya familia yangu akidai kuwa amekuwa akipigwa vita mara kwa mara na mwanangu. Sasa hivi sijui aliko kwani aliondoka jana.”

Alipopigiwa simu, bi Noel alilalamika kuwa mumewe anapaswa kumpigia simu moja kwa moja ila sio kupitia Radio Jambo.

“Huyo Tom tunakosania mamabo ya fitina na watu wao, sasa nitaishi aje na watu ambao hawanipendi? Kuanzia watoto wake aliozaa hawanipendi na hayo ndio maneno yananishinda.” Alisema Noel.

PATANISHO: Mke wangu ni wale wamelelewa kama paka ya duka

Aliongeza kuwa anakereka na kuogopa kuwa anaweza pangiwa mambo mabaya na isitoshe mumewe huambiwa mambo kumhusu na anaogopa pia yeye anaweza kumuumiza.

Kulingana na Noel, mumewe anapaswa kumpeleka kwao nyumbani kwanza ili amtambulishe kisha anunue shamba mahala kwingine ili awache kusumbuliwa. Tom kwa upande wake alimhakikishia mkewe kuwa atampigania na kuhakikisha kuwa hatosumbuliwa tena

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments