PATANISHO: Tulikosana Na Mke Wangu Baada Ya Kupigiwa Simu Na Mwanadada Mwingine

Jack mwenye umri wa miaka 34, aliomba apatanishwe na mkewe Josphine.

Tulikosana na mke wangu tarehe 27 Disemba alipotoka kutoka likizo ya Krismasi na kuondoka mnamo tarehe 21 Januari. Nilipigiwa simu na mwanadada fulani akiwa hapo lakini sikujibu.

Nambari hiyo ilikuwa ya ndugu yangu kitambo na nikama aliwacha kuitumia ikapatiwa mwanadada huyo." Alieleza Jack.

Nilijibu simu ile na mke wangu akakasirika sana na hata baada ya kufanya juhudi za kusuluhisho jambo hilo bado aliondoka. Pia nilijaribu kuita wazee na wazazi wangu wasaidie kusuluhisha jambo hilo, lakini wakanieleza ningoje kwanza ajifungue kwani alikuwa mja mzito.

Sasa amejifungua na siku niliyofaa kumuendea mwanadada aliniambia ashaendelea na maisha yake, na nisishughulike.

Alipopigiwa simu bi Josphine mwenye umri wa miaka 28, alijua tayari kuwa ni watangazaji, Gidi na Ghost.

Lakini alijitetea akisema kuwa mwanawe analia na alihitaji mda amlishe.

"Mke wangu hufanya hivyo ananiambia tarehe tutakayo patana kisha ananichenga. Mimi ndio nimemsomesha Josphine na kumlipia mahari na kumsaidia kupata kazi." Aliongeza Jack.

"Niko tayari kurudiana na bwana Jack iwapo atarekebisha swala la matusi na mipango ya kando." Alieleza Josphine.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be