PATANISHO: Wimbo Wa NASA Tibim Uliniharibia Ndoa Yangu!

Alfred alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Lorna baada ya wawili hao kukosana alipo hudhuria mkutano wa Chama naye na kugundua kuwa alikuwa na mpango wa kando.

"Gidi, ni uchungu na aibu. Mimi nilienda na Mke wangu na Dada yetu kwa mkutano wa Chama. Mke wangu hakuweza kuniheshimu. Kuna hii ngoma ya NASA kweli inanasa na inaharibu nyumba nyingi." alieleza bwana Alfred.

Merry go round ikaanza baadae nilikuwa nimetulia kwa kiti na mke wangu akaanza kufanya mambo ya aibu na mwanaume mwingine huku wakishikana wakicheza huo wimbo.

Alipewa pombe na baadaye akainuliwa nguo na wakatoka nje. Baada ya yale yote nikaita wazazi lakini hatukuweza kuelewana na akaelekea nyumbani.

Alfred ana miaka 35 huku Lorna akiwa na umri wa miaka 37.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 13, wamejaliwa watoto wanne.

Juhudi zetu za kumpata Lorna hazikufua dafu.

Kumbe jamaa huyo amekuwa na tabia za kutongoza wanawake wa wenyewe katika mikutano hiyo na hapo ndipo wanaume waliamua kumfunza adabu. " Alieleza zaidi bwana Alfred.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be