(+ Picha) Ghost Mulee na mkewe, ajivunia mapenzi yao ya miaka 27

Screenshot_from_2019_12_16_03_27_38__1576484892_15504
Screenshot_from_2019_12_16_03_27_38__1576484892_15504
Mtangazaji wa kituo hiki Ghost Mulee ameonyesha mapenzi kwa mkewe kwa kumpongeza kwa miaka 27 ya ndoa.

Katika mtandao wake maridhawa wa Insta, Ghost ameposti picha yake pamoja na mkewe na kusifia ndoa yao.

"Mungu wa maajabu kweli. Miaka 27 imepata ila nahisi kama jana tu..." Alisema Ghost.

https://www.instagram.com/p/B6FOnjqFyY4/

Sio mara ya kwanza Ghost kumshukuru Mungu kwa kuwaweka freshi na mke wake.

Ghost alikuwa kocha wa timu ya kitaifa ya Harambee na hatimaye akajiuzulu.

Katika mahojiano ya awali na kituo hiki , Ghost alisema kuwa kuchelewesha kwa mishahara kulichangia sana kujiuzulu kwake.

"Maswala ya kulipwa yalikuwa ni tatizo kubwa. Nawadai milioni kadhaa. Nimekuwa na rais wa shirikisho akanieleza kuwa wanakifa wataleta hela yangu kwa matanga haraka sana..."

&t=48s

"Kisa na maana cha kuacha kazi ni ushenzi wetu wa kutolipa watu pesa. Kuna wakati mmoja nimefanya kazi kwa miezi 8 bila kulipwa."

Ghost sasa anamiliki Liberty Sports Academy ambayo anaitumia kama sehemu nzuri ya kukuza vipaji.