(+ Picha) Othuol Othuol asimulia mahangaiko ya ulevi, mchango wa Churchill

Othuol-34-1-1
Othuol-34-1-1

Mcheshi wa Churchill Show Othuol Othuol amefunguka mwanzo mwisho kuhusu jinsi uraibu wa kunywa pombe ulimzidia na kupelekea kupoteza marafiki wake.

Nyota huyu wa ucheshi hayupo katika hali nzuri kiafya.

Kulingana na taarifa za vyanzo vyetu, Othuol ambaye ni mcheshi katika Churchill show amekuwa akipigana na kifua kikuu kwa kipindi kirefu.

Kifua kikuu kando, masaibu aliyoyapata kupitia unywaji pombe ni mengi mno.

https://www.instagram.com/p/BpOh_jMBrtZ/

"Hebu piga gharama ya kudaiwa kodi ya nyumba,kula vizuri na wakati huo uko mgonjwa?" Othuol aliuliza.

"Unaanza kuombaomba kiasi cha kwamba huwezi kuomba tena..."

https://www.instagram.com/p/BpOhzsvh1G3/

"Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakituma mchango wao na nafurahi sana..." Alisema Othuol.

Aidha, Othuol amesema Churchill amelipa pesa aliyodaiwa hospitali.

Othuol amesema kuwa uraibu wa pombe sio mzuri.

Amesema unaweza kuchangia kuwapoteza marafiki.