Proverbs 14:3: Aya ya bibilia ambayo Saphan alimtaka Eunice asome

proverbs (1)
proverbs (1)
Leo katika kitengo cha patanisho, Gidi na Ghost walikuwa na kibarua kigumu walipojaribu kuwapatanisha, Saphan na bi Eunice.

Kulingana na Saphan, mpenziwe wa miaka mitatu aliondoka kwa nyumbani baada ya kuzomewa na babake Saphan wakti ambapo alikosa kurudi nyumbani.

Kulingana na Eunice, babake Saphan hakutaka alale nje ya nyumba yake na wakti aliporudi alimfurusha kwa boma lake baada ya kumpa nauli.

Alimlaumu Saphan kwa kutomtetea mbele ya babake na alipopigiwa simu aliapa kutorudi nyumbani huku akimrai Saphan aendelee na maisha yake.

Kwa upande wake, Saphan hakuamini alichoskia na kusononeka. Aliapa kutomsahau mpenziwe hata kama itamchukua miaka kumi.

Wakti alipojua kuwa maji yamezidi unga alimuacha Eunice na aya mbili za biblia ambazo angependa azisome.

Hata hivyo aya iliyowafurahisha Gidi na Ghost ilikuwa ya mithali 14 mstari wa 3.

Aya hiyo inasema;

3. The proud speech of a fool brings a rod to his back, but the lips of the wise protect them.

Kiswahili:

Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi

Je wadhani baada ya kusoma mithali hii Eunice atamrudia Saphan?