Njura aliyekuwa kijana wa maka 19 wakati huo alimvusha Raila katika ziwa Victoria kuingia nchini Uganda wakati Bwana Odinga alipokuwa akisakwa na maafisa wa polisi . Njura wakati huo alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu na kwa kazi yake ya kumvusha Odinga hakujua mteja wake alikuwa nani na baada ya kulipwa shilingi 2000 kwa kazi yake ndipo alpojulishwa kuhusu ‘mteja’ aliyevushwa kuingia Uganda .
Kulingana naye ,baadhi ya vijana katika eneo hilo walikataa kumvusha bwana Odinga kwenda Uganda kutumia boti lakini yeye alijitolea . Odinga amesema mchango wa Njura katika kubadilisha mkondo wa siasa nchini kupitia hatua hiyo yake ni mkubwa na hauwezi kusahaulika .
Odinga ameandika ujumbe katika mitandao ya kijamii akimsifu Njura kwa hatua hiyo yake akisema ;
‘ Ni heshima kubwa kukutana na Robert Njura aliyenivisha kwa boti nchini Uganda nikienda mafichoni Norway .Njura ni dhihirisho kwamba ukakamavu ,kujitolea na nguvu za vijana kunaweza kuafikia mengi. Mungu ambariki pamoja na vijana wetu katika maadhimisho haya yam waka wa kumi tangu tuipate katiba mpya’ Odinga ameandika