Rais mustaafu Daniel Moi bado amelazwa hospitalini.

Rais Mustaafu Daniel Moi bado amelazwa katika Nairobi Hospital siku 20 baada ya kulazwa tena.

Moi alilazwa tena katika hospitali hiyo siku mbili pekee baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Katibu wake wa mawasiliano Lee Njiru wakati huo alisema kuwa rais mustaafu alikuwa anafanyiwa uchunguzi wa matibabu wa kawaida.

Tangu wakati huo Moi amekuwa hospitalini katika kitengo cha watu mashuhuri, chenye mandhari ya nyumbani ili kufanikisha uangalizi wa karibu wa madaktari.

Siku ya Jumatatu Njiru katika mahojiano ya simu, aliambia the Star kwamba Moi alikuwa chini ya uangalizi mkubwa wa madaktari, wakiongozwa na daktari David Silverstein.

Anasema kwamba Moi kwa sasa ameimarika lakini madaktari wanataka kusalia karibu naye ili kutathmini hali yake.

Hata hivyo alisema kuruhusiwa kwake kurejea numbani kutalingana na ushauri wa madakati.

"Mzee bado yumo hosptalini lakini anaendelea kuimarika. Tutatoa taarifa kamili kuhusu hali yake siku ya Jumamato. Kwa sasa tunafuata ushauri wa daktari,” Alisema

Njiru alisema kwamba taarifa hiyo itatolewa kama ni muhimu. Njiru hata hivyo alipuuzilia mbali uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba mzee ameaga na kusababishia familia yake masaibu.