Rotimi Asema alikuwa tayari kiakili kuwa katika uhusiano na Vanessa Mdee

Mwanamuziki wa Tanzania   Vanessa Mdee amekuwa katika uhusiano  wa kimapenzi na muigizaji wa  Hollywood Rotimi na sasa ufichuzi kuhusu uhusiao wao umeanza kujitokeza .

Wawili hao  walionekana hadharani mara ya kwanza katika ufuo wa Miami wakijivinjari  na kwa mara ya kwanza Rotimi amezungumzia uhusiano wao.  Akizungumza katika channel yake ya Youtube, Rotimi amesema ;

 “ Lazima uwe katika hali thabiti ya kifikira kama ya kuamua kuanza uhusiano. Watu wengi  hujiingiza katika mahusiano kwa sababu ya kuogopa kuwa wapweke. Hakikisha kwamba kwanza , kuna uliochoafikia peke yako kabla ya kuanza uhusiano na mtu.

 Unapokutana na mtu unayempenda, kila jambo linatitiririka bila kuhitajika kutumia nguvu au kulazimisha’

Aliongeza kusema

“ Unapompata mtu ambaye anayezidisha thamani kwako   basi ni vyema usalie naye  iwapo uko tayari’

 Kabla ya kukutana katika karamu moja huko Marekani  wawili hao walikuwa katika uhusiano na watu tofauti. Mdee alikuwa mpenzi wa msanii  mwenzake wa Bongo Juma Jux   na walikuwa pamoja kwa miaka kadhaa. Jux baadaye alimtambulisha mpenzi wake mzungu kutoka Thailand. Vanessa naye amekuwa akiishi Marekani na Rotimi .