Ruto aomba msamaha kwa 'mavazi yasiyo faa' katika tukio la mahakama

William Ruto
William Ruto
Naibu wa rais William Ruto ameweza kuomba msamaha baada ya kuvaa mavazi yasiyofaa katika tukio la mahakama lililokuwa katika mahakama ya juu Alhamisi.

Ruto alikuwa amevalia kanzu ya kijivu, shati nyeupe, suruali nyeusi na tai ya (Maroon) wakati mahakama ilipokuwa ikitoa ripoti ya mwaka 2017/2018.

"Ni furaha yangu kukuja na rais Uhuru mahala hapa, nikiangalia kila pande ni mimi tu pekee ambaye nimewachwa nyuma, kwa maana sijavaa mavazi yanayostahili,

"Nataka kumuomba msamaha jaji mkuu, nilikuwa nmevaa hivi nikienda katika tukio na mkutano mwingine lakini rais akaniuliza niweze kuja na yeye katika tukio hili," Alieleza Ruto.

Ruto aliweza kusema kuwa kuvaa mavazi yake haikuwa kutoheshimu mahakama, bali kuenda kwake katika tukio hilo ilikuwa kwa dharura na haraka.

Wageni wengi waliokuwa wamealikwa walikuwa wamevalia suti za rangu nyeusi, shati nyeupe na pia tai nyeusi.

"Hii si kuto heshimu au kutokuwa na heshima kwa kuvaa hivi, haina uhusiano wote na yale nilisema awali, lakini nataka kusema kwa heshima,

"Nina suala kubwa na mfumo wetu wa mahakama," Ruto alisema.

Naibu Ruto alisema kuwa mnamo mwaka wa 1988 aliweza kukutana na mwanachama mmoja wa mahakama, Paul Muite ambaye aliweza kukosoa serikali.

"Nikiwa na miaka 31 nilikuwa katika mstari wa kwanza ili niweze kutetea serikali, aliweza nipigia simu na kunishauri kuwa kuunga serikali mkono si vibaya lakini unapaswa pia kuikosoa,

"Kwa hivyo mnavyoona tunakosoa mahakama si kwa ubaya, bali kwa sababu tunaiunga mkono, wakati mwingine wanavyofanya vile hutaki ama hupendi ndio unaweza kutoka na kuanza kutoa maoni," Naibu Ruto aliongea.

Mwaka wa 2017 rais Uhuru Kenyatta aliweza kusema kuwa wataweza kukabiliana na wao na mahakama na kutembelea tena 'revisit'.

Hii ni baada ya mahakama ya juu kufutilia mbali uchaguzi wa urais wa mwaka huo.

"Niliweza shindia kusema kuwa tuna shida na mahakama yetu, tutaweza kupa heshima hukumu yao lakini tuta tembelea tena hukumu hiyo kwa maana tunafaa kuheshimu matakwa ya wananchi." Rais alisema.

Rais aliweza kuuliza mahakama iweze ijizoesha kuwa sawa.