Serikali yatoa mwongozo Miguna Miguna anatakiwa afuate ili kurejea nchini

oguna
oguna
Siku chache baada ya wakili mwenye utata Miguna Miguna kutangaza kurejea nchini, serikali imetoa mwongozo wa jinsi wakili huyu anatakiwa kufuata ili kuruhusiwa nchini.

Serikali imesema kuwa Miguna anatakiwa kuwa na stakabadhi halali za usafiri.

"Stakabathi zake za usafiri lazima ziwe halali na sawa. Kisha hatafungiwa kuingia. Stakabathi zake za usafiri ni lazima ziambatane na sheria za usafiri. Tunaongozwa na sheria," alisema msemaji wa serikali Cyrus Oguna.

Usemi wa Oguna unafuatia tangazo la wakili huyu mwenye uraia tata kuwa haogopi kusafiri nchini tarehe 11, Januari 2020.

Aidha, Miguna alichapisha nambari za dharura za watu wanaofaa kupigiwa iwapo kutatokea kizungumkuti katika safari yake.

Wakili huyu alifurushwa nchini mwaka jana baada ya tukio la kuapisha kinara wa chama cha ODM Raila Amollo Odinga.

Kwa sasa Miguna yupo nchini Canada na anapanga kurejea nchini baada ya kipindi cha miaka miwili.

"Ndege nitakayosafiria itatua uwanja wa JKIA tarehe 11,Januari 2020..." Ametangaza Miguna.