Sio mara ya kwanza John kutaka kujiua, Carol Paul asema

Screenshot_from_2019_12_12_13_17_33__1576145906_48067
Screenshot_from_2019_12_12_13_17_33__1576145906_48067
Ndugu wa mwanamume aliyekufa maji Bahari Hindi amefunguka na kusema kuwa sio mara ya kwanza John kujaribu kujitoa uhai.

Carol Paul ameongeza na kusema kuwa sababu za John Mutinda kujitumbukiza katika bahari kulichochewa na kuzongwa na fikra kwa kipindi kirefu.

Ndoa ya marehemu na Ruth Mueni ilisheheni matatizo tele.

Mutinda aliendesha gari lake kwa kasi baada ya kununua tiketi ya kuingia feri licha ya kusimamishwa na wathibiti wa kivuko hicho.

Mjane Ruth Mueni aliambia vyombo vya habari kuwa bwanake aliota kama amepigiwa simu na babake aliyefariki kitambo hivi kupelekea mauti yake.

Ruth alisema kuwa bwanake na babake walikuwa wapatane katikati mwa jiji la Mombasa.

Aidha, mamake John alikana taarifa hizo na kusema matatizo ya ndoa ndiyo yalichangia kijana wake kujiua.

“Mwanangu alifariki kutokana na kuzongwa na fikra iliyosababishwa na mkwamba alikuwa ameingiwa na kichaa,” alisema mama huyo wakati wa mahojiano naatatizo yaliyokuwa katika ndoa yake. Ni vibaya mkewe kusema alikuwa punguani..." Mamake John aliifungukia Taifa Leo.