Soma ujumbe wake Hamisa Mobetto kwa Diamond baada ya kumkabidhi haya

Video vixen na mwanabiashara Hamisa Mobetto alimtumia staa wa bongo Diamond Platnumz na baba wa mtoto wake ujumbe wa kumshukuru hii ni baada ya kumkabidhi suti yake aweze kushona, suti hiyo Diamond alivalia katika harusi ya dada yake Esma.

Jumanne kupitia kwenye mitandao ya kijamii Hamisa aliposti pucha ya Diamond akiwa amevalia suti ya maroon na kumshukuru kwa kumpa mkono katika kazi yake ya kushona huku akimuomba Mungu ambariki na baraka tele.

“Thank You for your Endless support, Ubarikiwe zaidi na Zaidi 🙏🏾🙌🏽. Good News Sasa Tunashona Suits za Kiume Classy & Unique .✨ Karibuni sana. kwa maelezo zaiid tafadhali Tupigie kwa Simu number . +255 677667788 💕 Tupo makumbusho opposite millenium tower." Aliandika Mobetto.

Haya yanajiri masaa chache baada ya Diamond kuposti picha yake na kutangaza kuwa Hamisa alitengeneza suti.

“Hakika Ilikuwa ni siku ya Faraja... Shukran kwa vazi hili la pili ..... & WEDDING ."

Mnamo tarehe 18 JUlai pia Hamisa alimshonea Dangote nguo alilokuwa amevalia katika hafla ya msanii Zuchu.

Awali Mobetto alisema kuwa siku hizi wanawasiliana sana na Diamond si kama vile walivyokuwa wanazungumza baada ya kuachana.

“Kwanza Kabisa kila mtu inafaa ajue kwamba mimi na Diamond tunaonge sana, tunaonana sana. Nikiwa labda na wazo la Biashara ananishauri, akiwa na jambo lolote anaomba ushauri, kwa hivyo tunaona na kusapotiana hapa na pale.

Lakini swala la Ndoa ni kitu ambacho kiko very sensitive, unajua Ndoa inapangwa na Mwenyezi Mungu and I don’t know what the future holds. So sina jibu sahihi kwa hilo swali." Alisema Mobetto.