Systema ya majambazi! Mahakama yataka Echesa apewe gari lake

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa anatarajia kuregeshewa bunduki na gari  vyote vilivyochukuliwa kutoka nyumbani kwake mtaani Karen, Nairobi kwa madai ya ufisadi.

Uamuzi uliotolewa na korti Alhamisi Juni 4, uliafikiwa baada ya kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) ikitaka Bw Echesa kuregeshewa bastola aina ya Beretta 92, Ceska na Range Rover yenye nambari za usajili KCR 786H.

Kupitia kwa wakili wake Bryan Khaemba, aliyekuwa waziri huyo alikuwa amelalamika kwa kusema kusafiria vyombo vya umma kulikuwa kukimweka katika hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya Corona.

Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani, Kennedy Cheruiyot katika uamuzi wake pia alifahamishwa bastola 2 zilikuwa sehemu ya ulinzi wa Echesa kutokana na hadhi aliyonayo ya uheshimiwa.

Katika uamuzi huo, hakimu Cheruiyot aliskiza na hatimaye kushawishiwa vya kutosha kuwa, malalamiko ya Echesa yalikuwa ya kweli.

"Nimeshawishiwa kuwa mlalamikaji ana haki ya kumiliki bunduki na kuruhusiwa kuwa gari lake," jaji aliamrisha.