PATANISHO: Mimi ndio hupigwa katika ndoa ya wake watatu

Taiti, 35, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Ernest, akidai kuwa wawili hao wanashinda wakikosana kila wakati akidai kuwa amefika mwisho na hajui la kufanya.

PATANISHO: Mke wangu hunidanganya kuwa mpango wa kando ni cousin yake

“Tulikosana Alhamisi wiki iliyopita kwani alienda kunywa pombe na wazee wenzake na akarudi na makelele, akanipiga karibu anichome na stove na hapo nikaondoka na kwenda nyumbani.” Alisimulia akisema kuwa mumewe ana wake watatu.

Stima ilikuwa imepotea na nikaondoka kwenda kununua mafuta ya taa, kurudi nikampata amesimama kwa mlango na kumuuliza mbona hajavalia nguo, akadai namuongelesha vibaya.

Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Hapo alichukua stove na kutupa na ikabaki nikizima moto.” Aliongeza akisema kuwa licha ya hayo yote bado anampenda na angependa kumrudia.

Isitshe Taiti alificchua kuwa mumewe huwa hapigi wake wengine ila yeye.

Bwana Ernest alisema kuwa wawili hao wanakosana tu kwa mambo ya ulevi na kuwa wawili hao ni walevi.

“Tulipokosana tulikuwa walevi pamoja na tulikuwa tunapiga story nikimwambia kuwa nitaongeza mke wa nne. Hapo akakasirika kwani hakujua ni mchezo.” Alijitetea.

PATANISHO: Ukibadilika nitajua tu kwani CCTV Ni mob

PATANISHO: Ukibadilika nitajua tu kwani CCTV Ni mob

Baba Mary belle aliomba apatanishwe na mkewe bi Mary belle, akidai walikosana tena na angepata apatanishwe.

Tulikosana mwezi ulioisha baada ya kwenda nyumbani na kumkosa. Nilipompigia simu aliniambia kuwa nafaa kufanya urafiki na pombe.

Sinywi pombe nyingi lakini si unajua mwanaume lazima apanguze vumbi akitoka kazini.

Sijamuoa ki rasmi kwani mimi ni generation ya microwave na ilikuwa tu ile ya come we stay.

PATANISHO: Sina wanawake wengine hao ni ma customers!

Jamaa ana miaka 29 huku mkewe akiwa na miaka 23. Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitatu na tayari wana mtoto mmoja.

Anajua chenye alinifanyia na awachane tu na mimi, alisema mama Mary belle. 

Hata kama mungu aliamua tuwe pamoja hakuna mahali ali sign. Wewe ile time utawacha kuoa pombe na marafiki zako utanitafuta na ukibadilika nitajua kwani CCTV ni nyingi.

Alisema Serah akisisitiza kuwa mumewe akibadilika atarudi.

Mumewe aliongeza kuwa alianza kubugia pombe kutoka akiwa kidato cha pili na ameshindwa kuwacha kwani yeye hunywa akisombwa na mawazo.

PATANISHO: Mume wangu hutaka tufanye mapenzi hadi nikiwa na periods

 

PATANISHO: Sina wanawake wengine hao ni ma customers!

Diana alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Nicholas.

Ni mambo tu ya nyumba shida kidogo kidogo kutoelewana akija kwa nyumba tunagombana na ananiambia nitoke niende.

PATANISHO: Mume wangu hutaka tufanye mapenzi hadi nikiwa na periods

 

Sasa nikaona haya maneno ya kuambiwa uondoke kisha unafanyiwa maneno sitaki na nikaamua niondoke. Nili time siku moja ameenda job na nikafunganya virago na kuondoka wiki mbili zilizopita.

Siku moja alinipigia simu kuuliza niliko na nikamwambia yeye ndiye alinifukuza na kuwa hafai kuuliza niliko.” Alisema Diana.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minane na hawajaliwa watoto. Diana anasema kuwa wakati bwanake alikuwa anataka mtoto yeye hakuwa tayari na sasa anavyotaka watoto mumewe hakuwa anataka.

Patanisho: Mpango wa kando wa bibi yangu anampigia simu tukiwa tumelala

Isitoshe wawili hao wana watoto kupitia ndoa tofauti lakini wanawashughulikia pamoja.

Bwana Nicholas alipopigiwa simu alisema;

Makosa ni yako kulingana na venye unaniongelesha, huwezi amini maneno ya simu bila evidence unaniwekelea vitu sijafanya na ndio maana nimekasirika.

Mimi nimetulia tu halafu nikifikiria nitakuambia.

Hata hivyo bwana Nicholas alikiri kuwa hana mipango ya kando kwani wanawake anaozungumza nao ni wateja wake.

PATANISHO: Ndugu yangu alihepa majukumu ya kuwasaidia wazazi

PATANISHO: Mume wangu hunidunga visu tukipigana

Monicah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe baba Jeff, ambaye walikosana mwezi mmoja uliopita na wawili hao hawazungumzi, isitoshe mumewe alimwambia kuwa atamuua.

PATANISHO: Naogopa mke wangu anaweza nyakuliwa

Tulikosana mwezi uliopita tarehe 21 na nimekuwa nikimshuku ana mpango wa kando na isitoshe amekuwa wa kunidunga na visu kila mara tunapigana.

Every Thursday huenda kazini na harudi kwa nyumba, kumpigia simu nikaskia echo na nikamuuliza kama yuko kazini kwani sikuskia mlio wa magari.

Sasa akanikelelesha akiniambia namchunga na akaniambia tupatane kwa nyumba eti nitamtambua. Kufika akanipiga na mshipi huku akisema kuwa nafaa kuhama na watoto. Alisimulia akisema kuwa anashuku hana mpango wa kando wala alioa bibi mwingine.

PATANISHO: Nilikuwa nimeolewa kwa familia iliyokuwa inalea nyoka

Monicah na mumewe wamekuwa kwa ndoa ya miaka na saba na wamejaliwa watoto wawili huku mmoja akiwa kidato cha tatu na mwngine akiwa darasa la sita.

Mwanadada alisema kuwa amejaribu kumuongelesha na ameshindwa isitoshe hamna yeyote anayeskiza na amejaribu kila juhudi na ameshindwa.

Juhudi zetu za kumtafuta bwana Ken hazikufua dafu.

PATANISHO: Mwanangu hana heshima yeye hunitusi mbele ya mke wake

PATANISHO: Naogopa mke wangu anaweza nyakuliwa

Bwana Austin Mukunda, 32, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Lilian, 32, ambaye walikosana mwaka mmoja uliopita.

“Vile alienda kwao alikwamilia huko na wazazi wake wanasema hadi niende kwao ndio atarudi. Sahii sina pesa kwani nina fanya biashara ya bodaboda na huwa hainipatii fedha.

PATANISHO: Nilikuwa nimeolewa kwa familia iliyokuwa inalea nyoka

Msichana aliniomba fedha za nywele na sikuwa nazo, hapo alinitishia kuwa ataondoka na kimchezo mchezo tu nilipata ameondoka.” Alijitetea Austin.

Wawili wao wamekuwa kwa ndoa ya zaidi ya miaka kumi.

“Wacha niishi na wazazi kwanza nione vile watasema halafu nitakujibu.” Alisema Lilian alipopigiwa simu licha ya Austin kudai kuwa amekuwa akikonda kwa kukosa mke nyumbani.

PATANISHO: Mwanangu hana heshima yeye hunitusi mbele ya mke wake

Lilian alisisitiza kuwa bado anampenda mumewe na kuwa atarudi kwake akishazungumza na wazazi na kuwa yuko tayari kungoja hadi mwezi wa sita.

Austin naye woga wake ni kuwa mkewe atanyakuliwa kwani wawili hao wameishi pamoja na wanaelewana ki tabia.

Nakupenda sana  I love you kama sweet water.” Alieleza Austin.

PATANISHO: Mwanangu hana heshima yeye hunitusi mbele ya mke wake

Boniface alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mamake mzazi ambaye walitengana na babake miaka kumi na mitano iliyopita.

“Mathe waliwachana na fathe na mimi pamoja na ndugu zangu sita tukaenda kwa wazee wa kijiji ili tuweze kumrudisha nyumbani. Kwenda kwa babangu alikataa kurudi nyumbani akisema kuwa walitengana na hayo yakaisha.

Baba yetu naye alituweka ndani na tulipotoka tuling’ang’ana na tukaweza kumrudisha mama nyumbani na tukamjengea nyumba.” Alisimulia Bonny.

PATANISHO: Nataka kujiua baada ya mke wangu kunipata na jirani kitandani

Alikiri kuwa baada ya mda mama yao alianza kuwabagua watoto wake kulingana na mali anayompelekea akidai kuwa sahii anaskizana na ndugu yake mkuu.

Ndugu yangu alikuwa anapeleka mahari na tukimzindikisha hapo ndio mathe alianza ugomvi nami, alilaani kazi yangu na watoto wangu sasa sielewi shida iko wapi.

Mama Beatrice alipopigiwa simu alisema kuwa mwanawe alimtusi vibaya sana mwaka jana jinsi bwanake alimkataa na kuwa ataleta gari itakayompoteza.

“Huyu hata akipata akienda haja ndogo napitanga kwangu lakini sasa anapitia huko kando ili aende haja ndogo, sasa mimi naye nani ana makosa, Mimi ndio nilimzaa mbona nimsingizie kuwa alinitusi?” Alisema Mama.

PATANISHO: Mteja wangu ndiye aliniharibia ndoa

PATANISHO: Nataka kujiua baada ya mke wangu kunipata na jirani kitandani

James, 39, alituma ujumbe akisema mke wake bi Diana, alimpata kitandani na msichana wa jirani na kuondoka kwenda kwa dadake. Alisema kuwa ameshanunua kamba ya kujitia kitanzi na tayari ameandika barua ya mwisho.

PATANISHO: Mteja wangu ndiye aliniharibia ndoa

Alipopigiwa simu James alisema kuwa shetani ndiye alichangia yeye kuwa na mpango wa kando, huku akisema macho yaliona na mwili ukapenda.

Msichana ambaye alipatikana naye ni wa umri wa miaka 27 huku mkewe akiwa na miaka 31.

“Huyu msichana nimemjua kwa siku kiasi tu na si eti tulikuwa tumefanya chochote hadi iyo siku. Sikuwa najua mke wangu atarudi kwani haikuwa masaa yake ya kurudi.

Niliskia mlango umebishwa na kufungua ni yeye na nilishtuka niki wish dunia inimeze kwani hakukuwa kuzuri.” Alijieleza James.

Patanisho: Hii ni siku yangu ya mwisho kwa ndoa ikiwa hutanipatanisha

Wawili hao wana mtoto mmoja katika ndoa ya miaka saba.

Alipopigiwa simu bi Diana, alisema kuwa mumewe alimuudhi ndio maana hataki kuzungumza naye.

“Aliniudhi ndio maana staki kuongea naye, hito nishamaliza najipanga chuma yake iko kwa moto atajua mwenyewe na narudi najua kile nakuja kufanya.” Alisema Diana.

Mwambie amechelewa na anafaa kuharakisha.” Aliongeza akisema kuwa hiyo ilikuwa mara ya kwanza mumewe kuwa na mpango wa kando.

Alisisitiza kuwa hataki kuzungumza na mumewe huku akisisitiza kuwa ndoa yao imeisha.
Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Mteja wangu ndiye aliniharibia ndoa

Fred alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Rael ambaye walikosana miezi miwili iliyopita.

Patanisho: Hii ni siku yangu ya mwisho kwa ndoa ikiwa hutanipatanisha

 

Mimi huwa mtu wa bodaboda na kuna alikuwa ananipigia ili nimpeleke sokoni kila siku, ikawa ananipigia simu hadi usiku nimuendee. Mke wangu ambaye anamjua akaanza kunung’unika akisema kuwa tuna uhusiano.

Siku moja yule msichana akanipigia simu na mke wangu kitu saa mbili akanipigia simu akisema kuwa ameondoka na kuwa nafaa kubaki na yule mwanadada ninayempenda. Aliongeza akisema kuwa hakuwa na uhusiano wowote na yule mwanadada.

PATANISHO: Karibu nimuue ndugu yangu lakini damu ni nzito kuliko maji

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja katika ndoa ya miaka miwili.

Alikuwa na rafiki ambaye alikuwa anamchukua na boda kitu saa kumi usiku na hapo nikaamua niondoke. Nikama walikuwa wanaelekea mahala kwingine kwani saa kumi wanaenda wapi? Aliuliza Rael akisema kuwa kila alipouliza alikuwa anagombanishwa.

Bwana Fred naye alikiri kuwa amewachana na yule mteja kwani amegundua kuwa anamharibia ndoa yake.

Rael alikubali msamaha wa bwana yake na kukiri kuwa atarudi nyumbani ili walee mtoto wao.

PATANISHO: Karibu nimuue ndugu yangu lakini damu ni nzito kuliko maji

Victor aliomba apatanishwe na nduguye mkuu bwana Moses, ambaye walikosana tangia mwaka uliopita. Isitoshe alikuwa amepanga kummaliza lakini sasa hivi anataka wawili hao wasameheane.

PATANISHO: Mama mkwe anataka kunipiga ili kulipiza kisasi

By the way ilifika mahali nikataka kummaliza kwani niliona nikama wanacheza na maisha yangu. Boma yetu ni ya mama tofauti ya watoto nane.

Nilitaka kukata mti ili nipate fare niende Nairobi na huyu ndugu yangu wa tumbo moja alizuia kwani ni shamba la familia na hilo ndilo lilileta shida. Alisimulia Victor.

Tumekuwa tukitishiana maisha kwani ndugu zangu walianza kunitafuta na sikuwa na lala wala kuishi na amani kwani tulianza kutusiana kwa simu.” Aliongeza akidai hafurahishwi na jinsi mambo yalivyo.

PATANISHO: Mke wangu alisema amepata jamaa mwenye fedha kuniliko

Bwana Moses, 39, alipopigiwa simu alimwambia Victor abadilike kwani amekosea wengi nyumbani.

“Wewe tu nakusamehe na ukija nyumbani njoo tuseme mawili matatu lakini mimi nilikusamehe kitambo.” Alieleza Moses.

Kulingana na Victor, alikuwa ameita vijana ambao walikuwa wamepanga kummaliza nduguye lakini wakati ulipofika alishawishika kubadilisha mipango kwani damu ni nzito kuliko maji.

 

PATANISHO: Mke wangu alisema amepata jamaa mwenye fedha kuniliko

Odhiambo, 28, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Jacqueline, 26, baada ya kumpiga na mkewe kukusanya virago vyake na kuondoka.

PATANISHO: Kila ninapokosa pesa mke wangu hunifukuza kwangu

“Najua nilikosa na na regret sahii. Ilifanyika last week on Wednesday.

Mke wangu hutokea kazi usiku sana na hiyo siku nilipata mtoto kwa nyumba akilia, nilipompigia simu kumuuliza kama haji akasema haji na akanipigia mdomo.

Nikampigia mara tano huku akikata, aliporudi nikamuuliza mbona hakusema alipokuwa na akaniuliza kama alikuwa amebeba sufuria, hapo nikakasirika na nikamzaba kofi.” Alisimulia Odhiambo.

PATANISHO: Bwanangu hanitetei licha ya mateso ya wakwe zangu

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wamejaliwa mtoto mmoja.

Nilifanya uchunguzi na mahali yupo yuaishi na jamaa mwingine ambaye alisema kuwa ana fedha zaidi kuniliko.

Alipopigiwa simu bi Jacqueline, alifichua kuwa kuna maneno mengi ambayo mumewe amemtendea na kuwa hana haja ya kuyazungumzia hewani.

“Kuna time yenye nilikuwa nimefungua shop mahali na nikawacha juu ya huyu. Alikuwa anavunja simu yangu daily na ikabidi niwache ile job basi.” Alisema Jacqueline.

Hata nywele amekuwa aking’oa hata ukaona kichwa changu waweza piga nduru.” Alisisitiza akisema kuwa mumewe alikuwa anapenda waganga.

Akijitetea Odhiambo alisema hakuwahi tumia fedha kupitia uganga na kuwa kama angeweza sahii angekuwa billionaire.

PATANISHO: Carol akwende huko alivunja mayai ya upendo