Tazama jinsi urembo wa mwanao Diana na Bahati unazidi kukolea

Ama kwa hakika, ni wazi bayana kuwa mwanamziki stadi Bahati na mke wake Diana Marua 'hutengeneza' watoto wazuri sana.

Kupitia kwa mtoto wao wa kwanza Heaven Bahati na sasa huyu wa pili Majesty, ni wazi kuwa wawili hawa huwa hawafanyi kazi ndogo wanapojiotayarisha kupata mtoto.

.

Mtoto Majesty alizaliwa tarehe 14 mwezi wa nane, na kama jina lake 'Majesty' mtoto huyu alikaribishwa kifalme.

Kwa sasa mtoto huyu ana miezi miwili lakini anawavutia wengi sana.

Hebu tazama picha hizi! Nina uhakika utakubaliana nami kuwa mtoto huyu ameumbwa akaumbika.