"Tetesi za kumuua Ruto ni uigizaji. Anajaribu kufunika habari feki," -ODM

unnamed
unnamed
Cheche za maneno zimezuka ghafla kati ya Naibu wa rais William Samoei Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. Vita hivi vya maneno vilianza wakati na ambapo Raila Odinga alisema kuwa viongozi wanaochanga maelfu ya hela katika harambee kanisani wanafaa watokee na kuwaeleza wananchi chanzo cha pesa hizo.

Soma hapa hadithi nyingine:

Kijembe kama hiki kilimpata vibaya William Ruto na akaamua kumjibu. Ruto alisema kuwa Raila ni "mungu wa umaskini" na lengo lake kuu ni kuwafanya wakenya waishi maisha ya ukata ili wazidi kumfuata kila uchao.

Ruto aliahidi kuwa atahakikisha kuwa kiongozi huyu wa upinzani hatapata nafasi ya kufanya hivyo katika utawala wa serikali ya Jubilee. Baada ya masaa chache, katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna akamjibu kwa ukali kwa kusema kuwa Ruto amekuwa kichekesho kwa wakenya. Edwin aliongezea kusema kuwa naibu wa rais anajaribu kufunika habari zake feki za watu kulenga kumuua.

Soma hapa hadithi nyingine:

Edwin alisema kuwa jina la Ruto lipo katika kila skendo ya ufisadi nchini na kumtaka agome kuhubiri jina Raila Odinga anapozuru sehemu tofauti tofauti nchini na awajibike kufanyia wakenya kazi.

"Hatushangai kusikia Ruto anamtusi kiongozi wetu Raila Odinga... usambazaji wa mbolea feki ambayo iliathiri wakulima wengi nchini inamhusisha yeye na marafiki wake wa karibu." Alifoka Sifuna.

"Kazi yake ni kumsaidia Rais kutengeneza mazingira mazuri ya biashara na nafasi za kazi nchini ili asianze kubeba bunda la noti katika magunia katika harambee kudanganya watu wamuunge mkono."

"Tunashangaa sana. Malengo yake ni yepi? Kati ya kuigiza kuwa analengwa kuuawa na kutaka kuwafurusha mawaziri katika baraza." alisema Edwin.