#ToboaSiri: Nilinajisiwa Nikiwa Darasa La Pili Na Hakuna Anayejua (AUDIO)

Mrembo mmoja aliwashangaza waskilizaji wa Radio Jambo hapo jana alipoamua kuwa mjasiri na kufichua kuwa aliwahi najisiwa akiwa msichana mchanga sana.

Haya yalitendeka katika kipindi cha Mbusii na Lion Teketeke, katika kitengo kipya cha 'Toboa Siri'.

Kulingana naye, tendo hilo la kinyama lilitekelezwa na mwanaume wa miaka 40, takriban miaka ishirini na mitano iliyopita masaa machache alipotoka kanisani.

"Mimi nimekuwa na shida kwa miaka ishirini na mitano,nilinajisiwa nikiwa darasa la pili na hakuna mtu yeyote anayejua hayo maneno." Alisimulia mwanadada huyo.

Nilinajisiwa na jamaa wa takriban miaka arobaini hivi tukiwa mashambani ambapo nilikuwa naishi na nyanyangu. Ilikuwa siku ya Jumapili na tulikuwa tumerudi nyumbani kutoka kanisani.

Sasa jamaa yule akanituma maji na akadai nimpelekee kwake na hapo akapata nafasi ya kunidhulumu na kunitishia maisha.

Tangia siku hiyo maisha yangu yalibadilika na sikuwa na cheza na watoto wenzangu kwani nilikuwa najikunja kila siku. Aliongeza mwanadada huyo huku akifichua kuwa hata mpenzi wake wa miaka mitatu hana habari kuhusu yale.

Pata uhondo kamili.