TUNDA LA SUMU: Mwanaume 'Akwama' Akishiriki Ngono Na Shemejiye Mjini Nakuru

kukwama
kukwama
Kulikuwa na kizaazaa katika mtaa wa Tanners mjini Nakuru baada ya mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 56 “kukwama” alipokuwa akila uroda na shemejiye.

Mwanamme huyo ambaye ni baba wa watoto watano alifumaniwa katika chumba kimoja alichokodisha jana usiku na hapo akaanza kula uroda na dadake mkewe kabla ya wawili hao kukwama majira ya alfajiri.

Wasimamizi wa chumba hicho walivutiwa na kilio cha wawili hao ambapo walilazimika kuvunja mlango na hapo wakagundua kuwa wawili hao walikuwa wamekwama.

Margaret Nambwire  ambaye ni bibiye mwanamme huyo aliwaambia wanahabari kwamba mumewe amekuwa msherati na ndiposa aliamua kutafuta usaidizi wa mganga ili aweze kumnasa.

Baada ya kulipa ada ya shilingi 40,000 Nabwire aliweza kupata huduma za mganga mmoja na baada ya kufanya anachokielewa zaidi, mumewe alijipata katika kitendo hicho cha aibu mapema leo.

Nabwire alielezea kuwa mumewe aliondoka mjini Kisii wiki jana akidai kuwa ameenda jijini Mombasa kununua gari ikiwa ni baada ya wawili hao kuuza shamba.

Alisema kwamba ni jambo la aibu kuona kwamba mumewe alikosa kujali hatma ya familia yake na badala yake akafika mjini Nakuru kustarehe.

Aidha umati mkubwa uliwasili katika eneo hilo kuweza kujionea wawili hao ambao walifunikwa kwa leso na wasamaria wema ambao walifululiza hadi nyumbani kwa mganga huo.

Nyumbani kwa mganga huyo, wawili hao baada ya kupakwa mchanganyiko wa madawa na waganga wawili, waliweza kutengana huku wakiomba msamaha kutokana na kitendo hich cha aibu.

Kwa sasa mwanamme huyo ambaye baadaye alitiwa nguvuni na maafisa wa polisi anatakiwa kulipa ada kwa mganga huyo kwa huduma ya kuwatenganisha.