Ufisadi! Jamaa aagizwa kulipa serikali zaidi ya shilingi milioni 300

JIMMIE KIAMBA
JIMMIE KIAMBA
Vita dhidi ya ufisadi vimepigwa jeki kufuatia agizo la mahakama siku ya Jumatano kumtaka mshukiwa wa ufisadi kulipa serikali zaidi ya shilingi milioni 300.

Jaji wa mahakama ya ufisadi Hedwig Ong’undi alimwagiza aliyekuwa afisa mkuu wa fedha katika kaunti ya Nairobi Jimmy Kiamba kulipa serikali shilingi milioni 317 kwa kukosa kueleza vyema vile alipata mali yake.

Habari zaidi:

                         : 

                         :

Jaji huyo alisema kwammba tume ya maadili na kupambana na ufisadi ilibaini kuwa maelezo yaliotolewa na Kiamba kuhusu vile alipata mali yake hayakuiana na thamni ya mali anayomiliki.