Ufisadi ni kama mbwa ‘kubwa Nono’-Balozi wa Marekani Kyle McCarter.

Balozi wa  Marekani humu nchini Kyle McCarter amekuwa  mstari wa mvele kulaani visa vya ufisasi na uporaji wa mali nchini Kenya tangu alipoteuliwa katika wadhfa huo   tarehe 2 Januari mwaka huu

McCarter amekuwa akitumia mitandao ya kijamii na hasa Twitter kukashifu  viongozi wanaohusika na  wovu wa kupora mali ya umma bila kujali mustakabali wa wakenya .  Hata hiyo miongoni mwa jumbe zake hizo la kulaani ufisadi ,ujumbe aliotuma katika Twitter  kwa lugha ya Kiswahili umepokelewa kwa  hisia tofauti huku  baadhi ya  watumizi wa twitter wakimkejeli kwa   kuvuruga ngeli na matumzi ya maneno ya Kiswahili lakini wengi wakimsifu wa ukakamavu wake kujaribu kuwasilisha ujumbe wake kwa lugha ya Kiswahili inayofahamika na wengi nchini .

Balozi McCarter sio mgeni kwa lugha ya Kiswahili kwani anaweza kuzungumza   Kiswahili  hata kuwaliko baadhi ya wakenya .Pia amechukulia ukosiaji dhidi yake kwa njia ya kistaarabu kwa kuahidi kujifunza zaidi .