Uganda yathibitisha visa vingine vipya 21

Taifa jirani la Uganda limethibitisha visa vingine vipya 21 vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya watu walioathirika na virusi hivyo kuwa 248.

Ripoti ya wizara ya afya ya taifa hilo imebaini kuwa watu hao wote 21 ni raia wa Uganda.

Watu hao walipatikana baada ya serikali ya Uganda kuwapima watu 1,071.

Mmoja wa waathiriwa ametokea katika mpaka wa Malaba.