Ugatuzi unaporomoka magavana waonya huku ukosefu wa pesa ukizua mgogoro

oparanya
oparanya
Ugatuzi upo katika hatari ya kuporomoka kwa sababu ya kucheleweshwa kwa fedha  a matumizi kutoka kwa hazina ya kitaifa .

Magavana wameonya kwamba mfumo huo wa  utawala huenda  hautastahimili  mgogoro wa ukosefu wa fedha  iwapo hakuna kitakachofanywa kwa haraka kubadilisha hali hiyo .

Hazina ya kitaifa bado haijatoa shilingi bilioni 32 zinzofaa kusamabzawa kwa kaunti kwa mwaka wa kifedha wa  2019-20.

Waziri wa fedha Ukur Yattani  hajatoa ratiba ya ni lin pesa hizo zitatolewa .

Kibaya zaidi ni kwamba kwa sasa kuna utata katika senate kuhusu  mfumo unaofaa kutumiwa kugawa pesa kwa serikali za kaunti  .

Kaunti nyingi hazina fedha na zimekuwa zikitumiwa shilingi bilioni 5  za kushughulikia janga la Covid  kuendesha oparesheni nyingine .

Kaunti haziwezi kugawana shilingi bilioni 316.5 zilizotengwa kwa mwaka wa kifedha wa 2020/2021 bila mfumo huo kuafikiwa .kucheleweshwa kwa mwafaka huo huenda kukazua matatizo zaidi kwa magavana .