Uhuru afungua uwanja wa Nyayo

Rais Uhuru Kenyatta  amefungua uwanja wa kitaifa wa Nyayo  baada ya ukarabati wa shilingi milioni 650 .

Uhuru  aliwasil katika uwanja wa Nyayo  saa sita kasorobo  kabla ya kufungua uwanja huo .

Rais aliandamana na waziri wa  Spoti Amina Mohammed  ,gavana wa Nairobi Mike Sonko na maafisa wengine wa serikali .

Uhuru  alitembea  katika uwanja  huo akionyesha  mageuzi yaliyotekelezwa  katika ukarabati .

Uwanja wa Nyayo  ulifungwa mwaka wa 2018 kwa ukarabati  ili kuandaa mashindano aya Chan  mwaka wa 2018  lakini mashindano hayo yakahamishwa hadi Morocco .

Rais Uhuru Kenyatta  aliiagiza wizara ya spoti  kuweka mikakati ya kuzuia utimizi wa dawa zilizoharamishwa  miongoni mwa wanaspoti .

" Tumekuwa na visa vya wanaspoti wetu kutumia dawa zilizoharamishwa  ingawaje visa hivyo ni vichache ,vinahofisha’ amesema rais

"  Toeni raslimali  za kuzuia utumizi wa dawa hizo  kwa kuzidisha uhamasisho ,vipimo  na kuripoti’

Akizungumza katika uwanja wa Nyayo rais amesema  sifa za Kenya katika  michezo zimejengwa kwa msingi wa kushiriki mashindano kwa njia ya kweli .

Uhuru amesema kufikia mwaka ujao maafisa wa KDF watakuwa na uwanja wao katika eneo la Langata