Ukoloni Mamboleo! Watanzania 2 watupwa baharini na Wachina kwa hofu ya kuwaambukiza Corona

SHIP-730x390
SHIP-730x390
NA NICKSON TOSI

Nahodha wa Mchina na wenzake katika meli ya kubeba mizigo wamekana madai kuwa waliwatupa watanzania wawili katika bahari iliyokuwa imejaa papa yaani shark Afrika Kusini kwa hofu kuwa Watanzania hao wangewaambukiza Corona, jarida la New York Times limeripoti.

Meli hiyo ilikuwa imewasili katika kivuko cha Durban, Afrika Kusini ikitokea Singapore mapema mwezi jana wakati ambapo wasimamizi wa meli kati ya watu 7 walipofahamu kuwa baadhi ya abiria wawili wa asili ya Kiafrika walikuwa wameabiri meli hiyo.

Jarida la Daily Mail limeripoti kuwa Wachina hao waliamua kuwapa vifaa vya kuwasaidia kupumua na mtungi wa Oksijeni na kuwaamuru kutoka kewenye Meli hiyo.

Waathiriwa Hassani Rajabu wa miaka 30 na Amiri Salamu wa miaka 20 wamesema walipewa vifaa hivyo kisha kuagizwa kutoka kwa meli hiyo.

Rajabu na Salamu wamekiri licha ya kufanyiwa unyama huo na Wachina hao fidhuli, hawakupewa chakula na mahali ambapo walirushwa kulikuwepo na papa, chui na wanyama wengine hatari.

Kwa bahati nzuri watanzania hao walibebwa na mawimbi ya bahari na kurushwa kwa kiziwa cha Zinkwazi karibu na Durban siku tatu baadaye.

Wakaazi wa maeneo haya baada ya kuwapata wakiwa hali mbaya waliwakimbiza hospitalini na kubainika kuwa walikuwa wameishiwa nguvu kutokana na njaa  na uchovu .

Baada ya Meli hiyo kutua katika mji wa Kwa Zulu katika kivukio cha Richards Bay, manahodha waliokuwemo ndani ya meli hiyo walitiwa mbaroni kwa unyama huo.

Rongli, Lin Xinyong, Zou Yongxian, Tan Yian, Xie Wenbin, Xu Kun Mu Yong wote walikana mashtaka ya kujaribu kuua mbele ya hakimu wa mahakama ya Durban Ijumaa Aprili 17.

Rongli alipigwa faini ya shilingi 537, 000) na wenzake kutozwa faini ya shilingi alfu 268, 000) kutokana na dhulma hiyo.