Utalijua jiji: Jamaa kawekewa ‘mchele’ na kuporwa kila kitu katika nyumba !

mchele
mchele
Kuna msemo kwamba Nairobi ina wenyewe na wakati umewadia kwa kila mtu kuwa mjanja ili kuweza kuishi katika mji huu bila matatizo ya kujitakia .

Mara nyingi umeskia kuhusu akina dada vibiriti ngoma wajanja kama  upepo ambao hupiga kambi katika baa na  maeneo ya burudani wakiwa na dawa za kulevya ambazo zinafanana kama mchele na wanakutilia katika kileo chako kasha wanakupora kila kinachokuita jina .  Basi jitayarishe kurudia stori kama hiyo lakini hapa kuna mhusika  na jina –Tobias hatosahau alivyokaribishwa Nairobi na nusra afe baada ya kuwekea dawa ya kumpoteza fahamu  na kupelekwa kwake na wanawake wawili waliosomba kila kitu katika nyumba yake mtaani Ruai .

Disemba tarehe 26 mwaka wa 2018 itasalia siku ambayo  Tobias kamwe hatowahi kuisahau kwa sababu baada ya usiku  war aha katika baa moja maarufufu mtaani Lang’ata aliamka tarehe 28 asubuhi akiwa amelala katika sakafu baridi ya chumba chake . Hapakuwa na chochote katika nyumba yake na Tobias alipata ugumu sana wa kujua iwapo alikuwa katika ndoto isioisha ama katika ulimwengu wa pili . Alipopata fahamu na kukumbuka yote yaliofanyika kuanzia siku ya krisimasi  ameweza kupata picha ya kilichofanyika na masimulizi yake ni kama movie .

Usimcheke ,mhurumie tu na pia ujasiri wake kueleza yaliyomfika iwe funzo kwa wageni wa jiji na waliozea jiji lakini hawalijui jiji . Krisimasi ilikuwa nzuri  na baada ya  kula  minofu mchana kutwa nyumbani pamoja na jamaa na marafiki ,Tobias alijua kweli amebarikiwa kufika disemba na hata kuisherehekea siku kuu ya krisimasi . Kesho yake tarehe 26 alikuwa bado na mchamcha za ulevi asijue atafanya nini lakini mpang ukatokea wakati binamu yake na rafiki zake kadhaa walipompigia simu ajifikishe katika baa moja mtaani Lang’ata ili wafanye ulevi na kubugia vileo kumaliza mwaka ..kwani iko nene? Maisha siku hizi ni kama ulaya na mara moja taxi ya kuitisha kwa simu ikafika na kijana kama starehe amejikalisha back left hadi katika baa hiyo .Muziki hapa ,densi kidogo na chupa zikajazwa mezani . Pembeni na kote katika baa kuna vipusa kweli ..wanawake warembo wa kila aina na kila wakati baadhi yao wangefika katika meza yao pale na kuwagusagusa ,kuwanengulia viuno kidogo na maisha yanapata utamu wake lakini filamu ndio ilikuwa imeanza !

Vileo vilianza kuwazungusha akili na wengine katika kundi lao wakaondoka kwenda makwao kupumzika ,Tobias na binamu yake walibakia pale ,gisa lilianza kuukaribisha usiku na penye giza ,ndio kuna mambo . Maskini katika meza yao ,vijana wale waliwakaribisha pia wanadada wawili warembo kupindukia na hata wakaitisha chupa kadhaa za vileo walivyotaka wageni wao katika baa .Kumbe wale sio wageni wa kukaribishwa bali waporaji ..kufupisha kisa  ni kwamba   Tobias na binamu yake waliwekea dawa za kuwalevya katika vinywaji vyao wakapoteza fahamu na kongea mambo yasioeleweka . Akiwa mlevi ,Tobias huwa haogopo kutangaza kwa sauti ya juu jinsi anavyofanya kazi na shirika la KRA!Watajuaje watu kuhusu kazi yake kubwa inayompa pesa nyingi kama  malipo? Pombe ina mambo!  Katika uleviw wake aliifungua simuu yake kuwaonyesha wanadada wale picha za  vyote vilivyo katika nyumba yake , kasema mipango yake ya mwaka ujao …kumbe pale  ndege kajiingiza mwenyewe mtegoni !

Walimbeba hadi nje wakaitisha teksi na kufululiza hadi kwake .walimtoa garini na kumpeleka hadi katika nyumba yake kabla dawa ile haijamponda kabisa .Kule nyuma walimuacha binamu yake Tobias bila fahamu na akiwa amezidiwa na sasa kalala kwa kuweka kichwa  chake mezani .  Mtaani Ruai  operation ‘pora mali’ ilikuwa ikiendelea .Wajanja wawili pale walimweka chini Tobias na kuitisha  lori pamoja na washirika wao .Walisomba kila walichotaka kutoka nyumba ile na kumuacha  mwenye nyumba na utajiri wa ulevi wake pekee . Kando na kumuacha hoi ,dawa walimpa nusra impotezee maisha mtoto wa wenyewe kwa sababu alipoteza fahamu kuanzia wakati huo  hadi asubuhi ya tarehe 28 wakati binamu yake alipokuwa kapatikana kwenye baa ,amepata fahamu na kuuliza alikokuwa Tobias . Karibu Nairobi .