TANASHA7__1___1561360136_69462

‘Vijana chipukizi wanaopendana,’ Mama Diamond asifia Tanasha

Mama ya Mwanamziki Diamond Platnumz amemsifia Tanasha Donna ambaye ni mpenzi wa mtoto wake. Mama Diamond ambaye anajulikana kwenye mitandao ya kijamii kama Mama Dangote alitoa sifa hizo kwenye Instagram na kuandika kwamba;

“Vijana Chipukizi, wanaopendana, wanyenyekevu tena wanaopendeza ❤❤❤”

tanasha.donna.diamond

Diamond alitangaza kwamba atafunga ndoa mwisho wa mwaka huu na mwanamitindo huyo wa Kenya huku akiisihi serikali ifanye siku hiyo sikukuu ya kitaifa.

Tanasha anadaiwa kuwa na mimba ya Diamond ila wawili hao hawajaweka wazi fununu hizo, lakini iwapo Tanasha ana Mimba, huyo atakua mtoto wa nne wa Diamond.

Diamond ana watoto wawili na aliyekua mpenzi wake Zari Hassan. Pia ana mtoto mmoja na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Diamond alipokua kwenye mahusiano na Zari, mamake alimsifia sana lakini sasa hivi, inaonekana kwamba Tanasha ndiye kipenzi cha mama mkwe.

Diamond akiri kumfuatilia Zari na mpenziwe katika mitandao ya kijamii

Photo Credits: Instagram

Read More:

Comments

comments