3A85AB8100000578-0-image-a-83_1479479846588

VIOJA TUPU! Mwanamume Akwama Akila Uroda Na Shemejiye Huko Nakuru

Kulikuwa na kizaazaa katika mtaa wa Tanners mjini Nakuru baada ya mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 56 “kukwama” alipokuwa akila uroda na shemejiye.

Mwanamme huyo ambaye ni baba wa watoto watano alifumaniwa katika chumba kimoja alichokodi jana usiku kushiriki ngono na dadake mkewe kabla ya wawili hao kukwama majira ya alfajiri.

Wasimamizi wa chumba hicho waliskia vilio vya wawili hao na kulaziika kuvunja mlango

Mkewe  mwanamme huyo aliwaambia wanahabari kwamba mumewe hajakua mwaminifu kwake na ndipo aliamua kutafuta usaidizi wa mganga ili aweze kumnasa.Anasema alilipa shilingi elfu 40 ili kupewa dawa hiyo ya mnaso

Mwanamume huyo anadaiwa kuondoka mjini Kisii wiki jana akidai kuwa ameenda jijini Mombasa kununua gari baada ya kuuaza shamba.

Wawili hao walifufuliza hadi nyumbani kwa mganga huyo, na baada ya kupakwa  mchanganyiko wa dawa , wakatengana

Kwa sasa mwanamme huyo ambaye ametiwa nguvuni na maafisa wa polisi anatakiwa kulipa ada  kwa mganga huyo kwa huduma ya kuwatenganisha.

Photo Credits: Files

Read More: Margaret Nabwire

Comments

comments