Patanisho: Mwanaume ataka kurudiana na mkewe baada ya kumpa dadake(15) mimba

Abraham alikuwa amempachika mimba mtoto huyo wa miaka 15 mara mbili, ya kwanza waliiavya na ya pili mtoto akafa.

Muhtasari

• Ruth alifichua kuwa mume wake alimpachika dada yake mimba mara mbili, ya kwanza ilitolewa, ya pili alijifungua mtoto akafa.

• Abraham alikuwa anawahonga polisi alipokamatwa kwa kumpachika mimba mtoto wa shule.

Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Ghost Mulee na Gidi Ogidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi cha Gidi na Ghost, kitengo cha Patanisho, mwanaume mmoja, Abraham Nyandieka alitaka kupatanishwa na mke wake Ruth baada ya kupatikana na mpango wa kando.

Abraham na mke wake walikosana miaka minne iliyopita baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka mitatu na kupata mtoto mmoja.

Mwanaume huyo alimtaka mkewe kurudi na kusema kuwa alikubali kuwa alikuwa na makosa na ndiye aliyesababisha wao kukosana.

 

"Anaweza kubali kurudi, nimeacha mipango ya kando. Sijaoa mwanamke mwingine baada yake, na yeye nina uhakika kuwa bada hajaolewa," Abraham alisema.

Mara ya kwanza, alikana kuwa baada ya kuachana na Ruth alioa mwanamke mwingine ila alikubali baadaye na kusema kuwa waliachana na huyo mwanamke kwa kuwa alikuwa na tabia ya kumtusi.

Ruth alipopigiwa alifichua yale yote ambayo Abraham hakuwa anaweka wazi.

"Anipe muda nifikirie, alinikosea sana hata nikianza kueleza ni aibu, mwambie awaeleze kila kitu, asiwafiche," mke wake alisema.

Abraham alifichua baada ya mazungumzo hayo kuwa alikuwa na mahusiano na dada ya Ruth mdogo ila aliwacha.

"Wewe ni kama shetani mkubwa, una uhakika hutarudia tena, hayo makosa ulifanya saa  hii ndo unaona ulifanya makosa, patanishwa na dada yangu, sina akili ya kururdi nyuma. Uliona sifai wakati huo," Ruth alisema.

Ruth alisema kuwa alimsamehe Abraham mara kadhaa baada ya kupewa ahadi za uongo.

Alifichua kuwa mume wake alimpachika mimba dada yake mdogo mara mbili huku akifichwa  kisha kumchomea nguo zake zote alipouliza.

"Akamweka dada yangu mimba mara ya kwanza nikifichwa, akatolewa mimba ya kwanza. Mimba ya pili akamweka mtoto wa huyo ambaye ni wa shule mpaka akafkuzwa shuleni," Ruth alieleza.

Alisema kuwa baada ya dada yake kuwa mja mzito alienda kuishi na mama yake mkubwa, kisha akazaa mtoto akafa.

"Dada yangu alikuwa ankufanyia nini ambacho sikuwa nakufanyia? Nina machungu bado. Alikamatwa ila alikuwa anawahonga mapolisi, mama yangu alijikakamua kutoa pesa ili afungwe ila alikuwa na pesa zaidi ya mama yangu,"mama huyo alisema.

Ruth alisema kuwa hata familia ya Abraham ilikuwa inamwona mbaya kwa kuuliza maswali kuhusu dada yake.

"Baba yake alinishikia panga kwa kuuliza swali tu," alisema.

Ruth alisema kuwa dada yake sasa ana miaka 15 ambapo ilibainika kuwa miaka minne iliyopita, alipopachikwa mimba, alikuwa na miaka 11.