Patanisho:Ndugu wakosana baada ya mmoja kudai baba ana majini

Paul na Jacob walikosana tangu mwaka wa 2017

Muhtasari

•Paul alikosana na ndugu yake mkubwa Jacob, mwaka wa 2017 baada ya Jacob kudai kuwa baba yao mdogo amefuga majini.

•Jacob alipigiwa simu ila hakuwa anapokea huku ndugu yake akisema huenda anaendesha pikipiki.

Ghost na Gidi studioni
Image: RADIO JAMBO

Jamaa anayejulikana kama Paul Ngure,33 kutoka Busia  alituma ujumbe akitaka kupatanishwa na ndugu yake mkubwa,Jacob mwenye umri wa miaka 38 baada ya kukosana  tangu mwaka wa 2017.

Paul alisema kuwa alikosana na ndugu yake takriban miaka saba iliyopita baada ya yeye kusema kuwa babake mdogo amefuga majini,ilhali ni uongo.Baba yao aliaga dunia na walikuwa wakilelewa na baba mdogo.

"Tulikosana na ndugu yangu mwaka wa 2017 na mpaka saa hii huwa hatuongei.Tulikuwa tunapendana kama mandugu wa tumbo moja.Alijiingiza kwa kanisa na kuanza kujifanya muombezi huku akidai kuwa baba wetu mdogo alikuwa na majini.Hio shida ilifanya mimi nikanunua shamba mbali na boma.Nudugu yangu yeye ako tu kwa boma upande wa Funyula"

Paul alisisitiza kupatanishwa na ndugu yake. "Nilikuwa naomba tuwe kimoja kwa kuwa ni ndugu yangu wa toka nitoke.Hata tukiwa na shughuli ya jamii ,hatuwez kaa pamoja..."

Aliongeza , "Issue kubwa ilikuwa,baba yetu mzazi alikufa,kulikuwa na baba mmoja ambaye ndiye kama kitinda mimba.Ikawa eti huyo baba yetu amefuga majini na anaua watu kwa jamii.Mimi nilikuwa naona kama ni uongo na hivyo kuleta utata kati yetu.Nilijaribu kumwongelesha akaona ni kama niko upande wa baba mdogo."

Jacob alipigiwa simu mara tatu ila hakuwa anapokea.Paul alisema kuwa Jacob alikuwa anaendesha pikipiki na huenda ndio sababu kuu ya kutopokea simu.

Mtangazaji Gidi alimshauri Paul kuleta mandugu au watu wa karibu  ili kuwapatanisha huku Paul akiulizwa ikiwa mama yao yupo.

'Mama yupo na pia alikuwa anachangia hio mambo,niliona kuwa hawezi tusaidia.Alikuwa upande wa Jacob..." Paul alisema.

Jacob alipigiwa simu kwa mara ya mwisho ila hakupokea. Je,una maoni gani kwa patanisho ya leo?