•"Nilikuwa namfariji tu nikimwambia kuwa maisha huwa hivyo na atapata mwingine. Mimi sikuwa nataka aone kama kwamba nampenda ama nataka turudiane. Sina hisia kwake," Bety alisema.
•Betty alichukua fursa kumuomba msamaha na kumhakikishia kuwa hana hisia zozote kwa mpenziwe wa zamani.
Betty, 23, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake John ,27, ambaye walizozana naye kuhusu ujumbe kwenye simu yake.
Betty alisema mumewe alichukua simu yake na kuona ujumbe wenye utata ambao alikuwa amemtumia mpenzi wake wa zamani.
"Ilikuwa wiki jana. Nilikuwa nikiongea ana ex kwa takriban wiki moja. Sikujua nitapatikana na sikuwa na nia mbaya," alisema.
Aliongeza, "Niliona ametengana na bibi wake wa miaka tatu. Nilikuwa namfariji tu nikimwambia kuwa maisha huwa hivyo na atapata mwingine. Mimi sikuwa nataka aone kama kwamba nampenda ama nataka turudiane. Sina hisia kwake,"
Betty aliweka wazi kuwa hana hisia zozote za kimapenzi kwa mpenziwe huyo wa zamani na kubainishwa kwamba hakuwa na nia ya kuvunja ndoa yake.
"Yeye (ex) alianza kuleta mjadala kuwa tunaweza kurudiana. Nilimwambia kuwa hatuwezi kurudiana kwa sababu mume wangu ananipenda na sina sababu ya kumuacha," alisema
Alisema kwamba alikuwa amefuta zake na ex wake kabla ya mumewe kuchukua simu yake ila ujumbe mmoja ulikuwa umesalia.
Ujumbe huo ulisoma, "Tafadhali, hii ndiyo meseji ya mwisho beb, mume wangu anatoka kazini."
Betty alisema kwamba mumewe aliweza kutambua namba hiyo kuwa ya ex wake licha ya juhudi zake kumdanganya kuwa ni ya mtu mwingine.
"Aliniambia amenisamehe lakini naona kama kuna kitu ameweka kwa roho," Betty alisema.
John alipopigiwa simu, Betty alichukua fursa kumuomba msamaha na kumhakikishia kuwa hana hisia zozote kwa mpenziwe wa zamani.
"Mimi nimeshakusamehea," John alisema.
Betty alimwambia mumewe, "Nakupenda sana na sikuwa na nia mbaya na sikuwa na nia ya kutoka kwa ndoa yangu niende kwa ex wangu. Pole sana. Nakupenda na nakuheshimu."