Vurugu zazuka katika makao ya Knut, Nairobi

KNUT
KNUT
Kundi moja la maafisa wa muungano wa kutetea walimu nchini Knut limevamia makao makuu ya muungano huo hapa Nairobi likitaka kuondolewa afisini kwa katibu mkuu wa muungano huo Wilson Sossion.

Maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia waliitwa kudhibiti hali ili pasizuke ghasia.

Sossion siku ya Jumatano aliagiza kufungwa kwa ofisi za Knut kutoka Agosti 28 hadi Septemba 3.

Knut awali ilikuwa imeahirisha mkutano wa baraza kuu la Muungano huo uliokuwa umepangiwa kufanyika Jumatatu 26 hadi leo.

Mkutano huo ulikuwa ujadili uongozi wa muungano huo ikiwemo mada ya kumng’atua ofisini katiba mkuu Wilson Sossion.