Picha za harusi ya Waiguru na mpenziwe Waiganjo

Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru anatarajiwa kufunga ndoa hii leo na mpenzi wake wakili Kimotho Waiganjo katika sherehe inayoendelea hivi sasa.

Sherehe ya harusi yao ambayo itakuwa ya kitamaduni itafanyika katika shule ya msingi ya Kiamugumo.

Waiguru alionya kwamba mambo ya kisiasa yasiingizwe katika harusi yake na Waiganjo huku akisema kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiyaingilia maisha yake na kuelta mambo ya kisiasa.
Wakili Wiaganjo anatoka Murang'a.