Wakenya wamzawadi nusu millioni jamaa aliyelazimishwa kulala na maiti ya mkewe

567c31b1d528fbf3
567c31b1d528fbf3
Wakenya wameungana na kumzawadi Charles Mwenda zaidi ya shilingi nusu milioni tangu kisa chake kilipoibuka mtandaoni,Mwenda ni jamaa aliyekuwa ametoka Malindi kuenda kumzika mkewe Meru na kwenye safari ya kupeleka maiti kaunti hiyo akakutana na maafisa wa polisi waliozima safari yake.

Waombolezaji wengine walitakiwa kurudi Malindi na yeye pamoja na maiti ya mkewe wakafikishwa kituo cha polisi alipolala usiku kucha.

Simulizi yake ya jinsi alivyoteseka katika kituo hicho, huku maiti ya mkewe ikinyeshewa bila ya kuwa na la kufanya iliwaguza wengi.

Mwanaharakati Ndung'u Nyoro alianzisha mchango mtandaoni na Jumanne, Juni 9 akatangaza kuwa KSh 570,469 zilikuwa zimechangwa kumsaidia Mwenda.

"Tunashukuru Mungu kwa kuruhusu uwe malaika kwa familia changa ambayo ilinyimwa nafasi ya kumzika mama na mke waliyempenda kwa heshima

Katika siku tatu, mmesaidia kuchangisha Ksh 570,469 ili kusaidia familia hiyo. Tunaomba kuwa fedha hizi ziweze kusaidia familia hiyo." Nyoro alizungumza.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko ni miongoni mwa wale walitoa mchango kwenye kampeni hiyo iliyokuwa imepewa jina la 'jaza kikapu'.

Mwenda alibaki na watoto watatu baada ya kifo cha mkewe Mwende.

"Asanti Gavana H. E Mike Sonko, kwa kujiunga na kampeni yetu ya jaza kikapu. Tulipokea mchango wako wa KSh, 25, 000 tuliupokea." Nyoro Alisema.