Wanafunzi 80 wa sheria chuo cha Nairobi wawasilisha kesi kupinga masomo ya dijitali

uon-law-campus
uon-law-campus
Wanafunzi 80 katika chuo kikuu cha Nairobi wanaosomea taaluma ya uanasheria siku ya Jumatatu waliwasilisha kesi mahakamani kupinga masomo ya dijitali ambayo yamependekezwa na usimamizi wa chuo hicho.

Kulingana na wanafunzi hao, hatua ya kuanza kutoa mafunzo kupitia mfumo wa dijitali haikuafikiwa. Wanafunzi hao vile vile walidai kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho wanaishi maeneo ambayo hawana uwezo wa kunufaika na mfumo dijitali.

 

Wamesema ni vyema chuo hicho kuendelea na mfumo wa kawaida ili kutoa mafunzo kwa wanafunzi wote.

“Mfumo wa dijitali hautatoa fursa ya kuwepo kwa mashauriano ya moja kwa moja baina ya wanafunzi na wahadhiri, hakuna nafasi ya kutosha kuingia maktabani na kufikia huduma zingine za moja kwa moja, na ingekuwa vyema kama karo ingepunguzwa,” walisema wanafunzi hao.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO