OLD BOXER

Wanaume msilale na chupi! Pia badilisheni na sio kuvalia moja kila siku

Wanaume wameshauriwa kulala bila chupi au kuvalia zinazolegea.

Mwanajinakolojia Allan Ikol anasema kuvalia chupi za kubana ni jambo linaloathiri kiwango cha mbegu zako za kiume na hata ubora wake.

Je,ni kipi kinafaa kutolewa bure? Kondomu au kisodo?

Ikol anasema uzalishaji wa mbegu huregemea kiwango fulani cha joto na sehemu iliyojibana huwa na joto jingi. Joto hilo ndilo linaloathiri uzalishaji wa mbegu za kiume. Anaongeza kwamba wengi hufanya kosa la kulala usiku wakiwa na nguo za ndani zinazowabana sana bila kufahamu madhara yake.

 

Pia kuna   hili tatizo la wanaume kuwa na tabia ya kuvalia chupi moja zaidi ya mara moja .  wengi hufikiri hatua hiyo haina madhara lakini    Dkt .Ikol anasema ,unajitia katika hatari ya kupata maambukizi  katika sehemu zako za  uume endapo utarejelea  chupi yako kila mara .Anasema  harufu  ,msuguo wa ngozi na jasho   ni mchanganyiko  unaoweza kusababisha ukuaji  bakteria hatari  inayoweza kukudhuru .

Ikol anasema sio ajabu kumwona mwanamme aliyejikwatua kwa suti nadhifu sana lakini  ndani ,Chupi ina matundu kama kichungi !

Je, ni kweli kwamba  wanaume  hawatalii maanani usafi wa chupi zao?

Kauli ya Siku Ijumaa 31 Mei 2019

Photo Credits: INTERNET

Read More:

Comments

comments