Watoto wangu wamenileta karibu sana na Mungu-Janet Mbugua

Aliyekuwa mwanahabari katika kito kimoja cha televisheni nchini Janet Mbugua aliongea kinagaubaga vile watoto wake wamemuezesha kuwa na uhusiano wa karibu na mungu.
Janet ambaye ni mkewe  Eddie Ndichu alisema maneno haya katika mtandao wa kijamii wa youtube.
Alisimulia na kusema,

"Watoto wangu wamefanya jukumu kubwa sana la kunileta karibu na mungu, na uwa nafikiria kuwa Huru na Mali  uwa wanawasiliana na hali yangu ya kiroho zaidi ya vile naweza," Janet alisimulia.

Mwanahabari Janet alikiri kuwa alipitia wakati mgumu na pia wakati mwema, lakini kwa sasa anataka kutenga muda sawa kwa majukumu yake yoye.

Janet pia alizungumzia aina ya wanaume vijana wake angetaka wakue waendapo kuwa wakubwa.
"Nataka wawe na fya njema, pia nataka waweze kueleza jinsi wanavyo jihisi wakiwa mahali salama, pia nataka kuishi kama kielelezo kwao," Alisema Janet.
Mwaka jana  alieleza sababu za kuacha kazi kama mwanahabari mashuhuri katika runinga ya Citizen.
Janet alisema kuwa alikuwa kama mgeni kwa mwanawe Huru kwa maana alikuwa anakaa na kulelewa na mfanyikazi. Hii ni kwa sababu alikuwa na ratiba ambayo ilikuwa imeshikana ya kazi.
"Kuna wakati nilienda kumkumbatia lakini alisonga nyumba, hakuwa ananifahamu vyema kwa sababu alitumia wakati wake mwingi na yaya," Janet alisema.

Ni jambo ambalo lilimfanya aweze kuamua maamuzi ambayo hayakuwa rahisi na kisha kuacha kazi yake.
Lakini baada ya kujiuzulu Janet alifanya hesabu ya pesa ya mradi ambao alikua anafanya kama pesa hizo zitamwezesha kujistahimili kimaisha kwa mda wa miaka miwili.