Watu 124 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo nchini Kenya

EZqr0faXkAIdoz8.jfif
EZqr0faXkAIdoz8.jfif
Chini ya saa 24 watu 124 katika taifa la Kenya wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo na serikali .

Kati ya visa hivyo wakenya ni 119, Wasomali wawili, mmoja kutoka Eritrea, na watu wawili kutoka Tanzania.

Visa hivyo vimepatikana baada ya serikali kuwapima watu 2640.

Mutahi amesema kuwa visa 26 ambavyo vimeripotiwa katika kaunti ya Busia  vimetokana na madereva wa masafa marefu .

Kufikia sasa kaunti ya Elgeyo Marakwet sasa imejiunga na majimbo mengine nchini yaliyoandikisha visa vya virusi hivyo.

Kagwe pia amesema kuwa wagonjwa wengine 39 wameruhusiwa kutoka hospitalini na kufikisha watu 592 waliopona .

Watu wengine wanne wamefarika na kufikisha watu 78 waliofariki kutokana na virusi hivyo.

Kwa sasa idadi ya wagonjwa wa corona nchini Kenya imefikia watu 2340.

Waziri wa afya pia amesema kuwa serikali imetuma bilioni 5 kwa majimbo yote 47 nchini ili kuweka mikakati ya kuanzaa kuwashughulikia wagonjwa wa virusi hivyo ambavyo hali yao si mbaya sana.

Kati ya visa hivyo vipya wanaume ni 100, huku wanawake wakiwa 24.

Kaunti ya Mombasa hii leo ndiyo iliyosajili visa 40 kati ya 124 huku kaunti bya Nairobi ikiwa na visa 38.

Kaunti ya Kajiada vile vile imeendelea kuandikisha idadi ya maambukizi huku wagonjwa wengine 6 wakiripotiwa hii leo.

Mutahi amewashutumu baadhi ya wakenya ambao wamekuwa wakiandikisha taarifa za uongo wakati ambapo wanaenda kufanyiwa vipimo katika vitu0 mbalimbali vilivyotengwa nchini.

Amewahimiza wakenya kuwa ange na kuwashtaki watu ambao wamekuwa wakitoroka maeneo ya karantini nchini.