Watu 168,464 bara la Afrika wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona

Shirika la afya duniani tawi la Afrika limethibitisha kuwa kufikia sasa watu 168,464 katika mataifa yote ya Afrika wameambukizwa virusi vya corona .

Wakati uo huo WHO imesema kuwa watu wengine 73,000 wamepona dhidi ya virusi hivyo huku wengine 4,700 wakiwa wamefariki.

Afrika Kusini ,Misri na Nigeria ndiyo mataifa ya kipekee Afrika ambayo yamesajili idadi kubwa ya maambukizi kufikia sasa.

Kenya kufikia sasa imeripoti visa 2,340 huku watu 592 wakiwa wamepona.