Watu 538 wapatikana na covid 19 huku 8 wakiaga dunia

Kenya leo imesajili visa vipya 538  vya ugonjwa wa corona  baada ya sampuli 6195 kupimwa katika muda wa saa 24 zilizopita .visa hivyo sasa vinafikisha jumla ya visa vya wagonjwa wa corona nchini kuwa 24,411 huku sampuli zilizopimwa zikifikia 335,318.

Katibu wa utawala katika wizara ya Afya Rashid Aman amesema  katika ya visa hivyo vipya  516 ni vya wakenya ilhali 22 ni vya raia wa kigeni .wanaume ni 333 huku wanawake wakiwa 205 .Mgonjwa wa umri wa chini sana ana miaka 2 huku wa juu zaidi akiwa  na miaka 85 .

Aman amesema Nairobi inazidi kuongoza kwa visa vingi baada ya  kusajili 277 ikifuatwa na Kiambu kwa visa 72.

Aliongeza kwamba watu 514  wamepona na kufikisha jumla ya idadi ya waliopona kuwa  10,444

Hata hivyo watu   wanane wameaga dunia na kufikisha jumla ya walioangamizwa na Covid 19 kuwa 399 .