Waziri mpya wa Elimu na Kamishna Mkuu wa Magereza waapishwa katika Ikulu

Rais Uhuru Kenyatta leo katika Ikulu ya Nairobi alishuhudia kuapishwa kwa Waziri mpya wa Elimu Profesa George Albert Omore Magoha na  Kamishna Mkuu wa  Huduma  ya Magereza   nchini Bw. Wycliffe Ogalo.

Sherehe hiyo ya kuapishwa iliongozwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma Bw. Joseph Kinyua.

Akimpongeza Waziri mpya wa Elimu kwa uteuzi wake, Rais Kenyatta alisema anatazamia kushirikiana naye pamoja na washikadau wengine katika sekta ya umma  ili kutekeleza  mtalaa mpya wa elimu na vile vile kufanikisha utaratibu wa kuhakikisha wanafunzi wote wanaofanya mtihani wa darasa la nane wanajiunga na shule za sekondari.

“Tunataka kuona ukiendela na marekebisho yanayotekelezwa. Tunaamini kwamba kuna uwezo kwa wewe na maafisa wenzako pamoja na wanaume na wanawake wanaohudumu chini yako kutambua jinsi wafungwa waliorekebishwa tabia wanavyoweza kuchangia maendeleo ya Kenya,” kasema Rais.

Waliokuweko wakati wa sherehe hiyo ni pamoja na  Waziri wa Masuala ya Ndani Fred Matiang’i, Mkuu wa Wafanyakazi na Kitengo cha Rais cha Kukadiria Utekelezi wa Miradi ya Serikali Bw. Nzioka Waita miongoni mwa maafisa wengine wakuu serikalini.