Nonini.Wyre.Nameless

Wikendi imefika watu waserereke! Orodha ya nyimbo za kuskizwa wikendi hii

Hayawi hayawi huwa! Wikendi kisha fika na ni wazi kuwa kila mtu anasubiri siku hii kwa hamu na ghamu haswa wakati huu ambao shule zimefungwa na watu wanataka kujiburudisha kwa nyimbo na mvinyo.

Hata hivyo,ninaamini kuwa sote tunajua kuwa kitu kikizidi kiasi huwa sumu aisee kila kitu kinafaa kufanywa kwa kiasi kwani kitumbua kikiingia mchanga mambo yataenda mrama.

Vilevile kwa vijana wetu lazima muelewe fika kuwa wahenga hawakuwa wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa waliposema asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu hivyo basi muwajibike muendapo kujiburudisha.

Amini Usiamini, Radio Jambo imewaandalia orodha ya nyimbo za kale ambazo ni bomba na unaweza kuziskiza kabla ya kuenda kwenye klabu au nyimbo za kumwambia Dj kwenye klabu akuwekee ili ujiburudishe kwani ya kale ni dhahabu!

1.Keroro

Mwanamziki Nonini aliimba nyimbo bomba sana ya kuenda kwenye klabu kama Keroro.

Adinasi wengi mpaka wa sasa wanajiburudisha na wimbo huu.

MacDonald Mariga atua Lindi, hana uwezo wa kujipigia kura

 2.Banjuka juu

Wimbo huu ni wimbo ambao uliwafurahisha watu wengi sana na hata mpaka sasa,wimbo huu unaweza kufurahisha wengi.

3.Under 18

Wimbo huu wa Under 18 wake Jimwat, ni wimbo ambao una mafunzo kwani mwanamziki huyu alikuwa anawapa mawaidha na kuwaonya vijana wanaoenda kujivinjari na mabiti wadogo.

4.Furahiday

Nonini na mwanamziki Nameless walitoa wimbo mufti sana wa furahiday kwani kwani wimbo huu uliwafurahisha wengi na uliimbwa sana katika vituo vingi vya kujiburudisha.

5.Mpaka Che

Wimbo mpaka che ulimbwa na mwanamziki bomba sana, Pilipili na Jimwat na pia uliwafanya wengi sana kujiburudisha.

(+ Video) Diamond Platnumz ampiga Ali Kiba chambo kali, BABA LAO

6.Kamata Dame

Kamata dame ulikuwa ni wimbo ulioimbwa katika klabu zote Nairobi na wengi walifurahia sana kusikiza mziki huu.

7.Jana Kuliendaje

Mwanamziki Mejja aliwaburudisha wengi na mziki wake ‘Kweli Jana Kuliendaje ‘ na ninaamini unaweza sadiki kuwa wimbo huu uliwafurahisha wengi sana.

8.Tonight

Kidosho Amani alitoa moyo wake wote katika wimbo huu kwani mziki huu wa Tonight uliwafurahisha wengi kwa kuwa ni binti alikuwa ameimba na pia ulikuwa  na ubunifu mkuu.

9.Ninanoki

Nameless mpaka wa sasa ni mwanamzki ambaye hutoa mziki ambao utawafanya wengi wanengue viuno.

Binti Amani na Nameless waliimba wimbo huu na kuwafanya wengi wapendane na kujiburudisha bila kupumzika.

10. Dondosa

Dondosa ni wimbo ambao ulikuwa unahimiza mabinti wanengue viuno vya na amini usiamini, wengi walinengua viuno vyao na kusakata kayaya za chini kwa chini.

Hata hivyo, kwa vijana wetu lazima muelewe fika kuwa wahenga hawakuwa wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa waliposema asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu hivyo basi muwajibike muendapo kujiburudisha.

Usisite Kurodhesha mziki wako ambao ulikuwa wa kitambona ulikuwa unawafurahisha wakati wa kujiburudisha.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments