Yanayomwandama Grace Mugabe yasimuliwa. Je, afuate yepi?

Wiki iliyopita ilikuwa ya misukosuko na simanzi kwa raia wa nchi iliyopo kusini mwa Afrika Zimbabwe.

Ndugu,jamaa na marafiki wa Robert Mugabe wamegumbikwa na wingu la majonzi baada ya Rais wa kwanza, shujaa na mkombozi wa taifa hili kufariki.

Katika mduara wa matukio hayo yote, mkewe Grace Mugabe yupo yupo.

Ukwasi alionao kwanza ni ishara kwamba mamlaka yana uwezo mkubwa sana.

Ila je, ni kati ya maswala gani yanayomwandama mama huyu wa taifa?

Grace Mugabe ni katibu aliyeolewa na Rais Mugabe.

Grace aligonga vichwa vya habari kwa hasira zake za mkizi.

Ununuzi wa bidhaa za bei ghali mno.

Kisomo chake cha juu kilimwezesha kuzamia katika siasa za Zimbabwe na kuongoza ligi ya wanawake katika chama tawala cha ZANU PF

Kipo kipindi mama huyu aliitoroka nchi yake na kufurushwa katika chama hiki.

Je, huenda watu hawaipendi hulka yake?

Kulingana na Patrick Zhuwao ambaye ni ndugu wa ukoo wao,

"Grace ni mkakamavu. Ataishi Zimbabwe. Kuna wale watamsaliti ila ataishi."

Mzozo uliokuwepo wa atakapozikwa Robert Mugabe haukumfurahisha Grace.

Wengi mpaka leo hawajui ni kwa nini Grace alikuwa katika mstari wa kwanza kukataa mazishi ya kitaifa ya mmewe.

Mengi pia yanasalia kizungumkuti iwapo Grace atazamia siasa za Zimbabwe.

Grace hawezi kuishi katika hali ya kuikimbia nchi yake.

Mwanzo lazima akae kikao na wakuu serikalini wapange utaratibu wa usalama wake, familia na utajiri wake malkia huyu.

Hatakuwa wa kwanza kufanya hivi kwani mmewe alisaini mkataba wa kusalia katika hali ya utulivu ya serikali hii.

Grace alipendekeza mwili wa bwanake ujengewe ukumbi wa ukumbusho.

Kwa sasa yupo na huenda akasalia katika jumba kuu la Blue Roof akiipatia serikali muda kukamilisha ujenzi wa makumbusho ya mmewe.