'YAUMA',Mke wangu aliniachia mtoto siku chache baada ya kujifungua

Katika Bustani ya Massawe Japanni leo mwanamume mmoja alipiga simu akilalamikia hatua ya mkewe kujifungua mtoto na kumuachia.
"Nilikaa na yeye kwa miaka miwili na tukaachana, lakini aliniachia mtoto hadi wa leo hataki kujua mtoto wake anaendelea aje," Alieleza mwanamume huyo.

Ni jambo ambalo lilifanya mashabiki wachangie na kila mmoja kutoa maoni yake, si wazazi wa kike pekee ambao wanaachiwa watoto bali hata wa kiume huachiwa wana na kuwalea bila usaidizi wa mama mtoto.

Yafuatayo ni baadhi ya maoni ambayo yalitolewa;

" Mimi niliacha mtoto wangu kwa babake akiwa na miezi mitano na sasa hivi ana miaka mitano anaenda shule sasa, nilimuacha kwa sababu huyo mwanamume alikuwa msumbufu sana," Alisema shabiki wa kwanza.

"Niliachiwa mtoto kwa sababu ya mzozo wa kifamilia na bibi yangu alienda kabisa," Shabiki wa pili aliongeza.

Wengi walipiga simu na kusema kuwa hawawezi kuacha mtoto wao heri waende na wao.

"Mimi siwezi muacha mtoto wangu heri niende na yeye".

Kweli waswahili hawakukosea waliposema kuwa uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi

Ni watoto wangapi wamewachwa na mama au baba zao? lakini cha kustaajabisha ni mzazi wa kiume kuachiwa mtoto na kisha mzazi wa kike kutoweka kabisa bila haja ya kumuona mtoto wake.

Inamaanisha kuwa hawapendi watoto wao ama tutasema kuwa hawana utu ndani yao wanapoamua kuwaacha wana wao?

Hata katika wakati huu wengi wanaacha huku wengine wakiwatupa na kuendelea na maisha yao kwingineko bila kujali.

"Niliachiwa mtoto akiwa na wiki moja lakini baadaye mamake akarudi na kumchukua," Shabiki mmoja alizungumza.

"Massawe hata mimi niko na mpango wa kumuacha," Mama mmoja alipiga simu na kusema.