'Kanisa ilikuwa sababu kuu ya kuachana na mume wangu,'Mtangazaji Joyce Gituro afichua haya

Muhtasari
  • Mume wangu alibeba kila kitu kwa nyumba na kutuacha
  • Nilipoteza mume wangu kanisani na hilo ndilo sababu kuu ya kuachana naye Joyce Gituro
  • Kuna siku pasta alisema tufunge milango na dirisha tufukuze mapepo
unnamed (13)
unnamed (13)

Mtangazaji wa kipindi cha jumapili cha Radiojambo Joyce Gituro kwa mara ya kwanza ameweka wazi nini haswa kilichochangia yeye kuachana na mume wake.

Joyce akiwa kwenye mahojiano alisema ya kwamba waliachana na mumewe baada ya kuwa kwa ndoa kwa miaka mingi.

Mama huyo wa watoto watatu alisema kwamba shida ilianza pale mumewe alibadilisha kanisa walilokuwa wanahudhuria.

 

"Kanisa ndilo lilikuwa sababu kuu ya yangu na mume wangu kuachana, nilimpoteza mume wangu kanisani mume wangu aliniambia tutoke katika kanisa ambalo tulikuwa tunaabudu na kujiunga na kanisa ambalo si kuliamini

Nilipojiunga na kanisa hilo niliambia mume wangu siko sawa na mafundisho yao, kuna vile kanisa hilo lilikuwa 

Nakumbuka siku moja pasta alisema tufunge dirisha na milando ili tuweze kukemea shetani,nilimwambia mume wangu siko sawa niliwachukua watoto wangu na tukatoka nje

Nilipotoka pasta hakupendezwa na kitendo hicho na hapo ndipo shida ilianza,nilipozungumza na mume wangu aliniambia sikufanya vyema." Alieleza Gituro.

Mtangazaji huyo alieleza vile mume wake alibeba kila kitu na kumuacha,

"Mume wangu alituacha na kubeba kila kitu kwa nyumba sijawahi mwanamume ambaye anabeba jiko,jokofu na vitu vingine vyote vya nyumba

Nilishtuka sana, tulikuwa na shida zetu lakini sikutarajia itafika hapo."

Gituro alisema kuwa alianza kutambua jambo lisilo la kawaida kutoka kwa mume wake baada ya kupoke unabii usiowa kawaida kutoka kwa nabii huyo.